Maroni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Picha ya Kirusi ya Mt. Maroni.

Mtakatifu Maroni (kwa Kiaramu ܡܪܝ ܡܪܘܢ, Mar|Mār(y) Mārōn; kwa Kiarabu: مار مارون‎) alikuwa padri mwenye juhudi za kimisionari nchini Siria.

Ndiye mwanzilishi wa tapo la kiroho lenye jina lake ambalo lilizaa nchini Lebanon Kanisa la Wamaroni lililomo katika ushirika kamili na Kanisa la Roma na Kanisa Katoliki lote duniani.

Alifariki kati ya mwaka 406 na mwaka 423 akaheshimiwa kama mtakatifu.

Kuanzia karne ya 17, sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 9 Februari.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maroni kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.