Mkaapweke

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Paolo Uccello, Matukio ya maisha ya wakaapweke.

Mkaapweke ni mtawa aliyejitenga na jamii ili kuishi upwekeni na kusali tu.

Nje ya Ukristo[hariri | hariri chanzo]

Asia ilikuwa na maisha ya kitawa walau tangu karne ya 6 KK, hasa katika Uhindu na Ubuddha.

Katika Ukristo[hariri | hariri chanzo]

Katika Ukristo asili ya maisha hayo ni jangwa la Misri katika karne ya 3 na hasa ya 4. Paulo Mthebani (+ 250 hivi) ni wa kwanza kujulikana.

Antoni Abati, mmoja kati ya wale waliovutiwa naye, alijivutia umati wa wafuasi kusini mwa Misri: kutoka huko wakaapweke walienea kote mashariki mwa Dola la Roma, hasa Palestina (Hilarioni wa Gaza) na Kapadokia (Basili Mkuu na Gregori wa Nazianzo).

Wengi kati ya hao wa kwanza wanajulikana kati ya mababu wa jangwani.

Baada ya Pakomi (+ 318 hivi) kuanzisha maisha ya kijumuia kwa watawa na kuwatungia kanuni ya kwanza, mtindo huo mpya ulizidi kuenea usifute kabisa ukaapweke.

Ukaapweke ulienea pia magharibi hasa kutokana na kitabu cha Atanasi wa Aleksandria juu ya Antoni na kile cha Jeromu juu ya Paulo; kuanzia karne ya 4 Afrika kaskazini magharibi na Ulaya pia walipatikana wakaapweke, hasa Gallia, Britania na Ireland.

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.