Sinodi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Sinodi ni mkutano wa Kanisa la Kikristo ambao huunganisha wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali za Kanisa au eneo maalumu ndani ya Kanisa kama sinodi.

Maana ya neno lenyewe katika lugha asilia ya Kigiriki (σύνοδος = sýnodos) ni kufuata "njia ya pamoja".

Kiasili sinodi ilikuwa mkutano wa maaskofu wa eneo fulani.

Wakati mwingine neno "mtaguso" hutumiwa kwa kutaja sinodi ya maaskofu wote, kwa mfano mtaguso mkuu ni mkutano wa maaskofu wote wa Kanisa Katoliki duniani.

Mara nyingi mkutano mkuu wa dayosisi au wa jimbo la Kanisa huitwa pia "sinodi".

Katika madhehebu ya Kiprotestanti sinodi hujumlisha wachungaji pamoja na walei.

Wapresbiteri hutumia neno "sinodi" kwa ajili ya mikoa yao ikitawaliwa na sinodi yaani mkutano wa wajumbe kutoka shirika.