Victoria (ziwa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Ziwa la Viktoria Nyanza
Ziwa Viktoria Nyanza jinsi inavyoonekana kutoka angani
Ziwa Viktoria Nyanza jinsi inavyoonekana kutoka angani
Mahali Afrika ya Mashariki
Nchi zinazopakana Tanzania, Kenya na Uganda
Eneo la maji 68,100 km²
Kina ya chini 81 m
Mito inayoingia Kagera, Katonga, Nzoia
Mito inayotoka Nile
Kimo cha uwiano wa maji juu ya UB 1,134 m
Miji mikubwa ufukoni Kampala, Kisumu, Mwanza
Ziwa Viktoria na Bonde la Ufa
Ongezeko la msongamano wa watu kandokando ya Ziwa Victoria
Lugha kandokando ya Ziwa Victoria
Tofauti ya levo katika Ziwa Victoria
Ongezeko la msongamano wa watu kandokando ya Ziwa Victoria likilinganishwa na lile la Afrika nzima

Ziwa Victoria (pia: Viktoria Nyanza, Ziwa Nyanza) ni ziwa kubwa katika afrika ya Mashariki lililopo baina ya Tanzania, Kenya na Uganda. Ni ziwa kubwa kuliko yote barani Afrika, na la pili duniani. Ziwa la kwanza ni Ziwa Superior ambalo lipo Amerika ya Kaskazini.

Ziwa Victoria lipo mita 1134 juu ya usawa wa bahari na lina eneo la kilometa za mraba zaidi ya 68,100.

Maji ya ziwa Victoria yanamiminika kwenye mto Nile na kuelekea bahari ya Mediteranea kwa umbali wa maili 4,000.

Ziwa hili linapata maji yake mengi kutokana na mvua (80%) na kutoka vijito vingi vidogo. Mto mkubwa unaoingia Victoria ni Mto Kagera unaotiririka kutoka magharibi.

Ziwa Victoria ni miongoni mwa maziwa yenye visiwa vingi vidogovidogo.

Ziwa hili lina kina cha wastani cha mita 40 na mwambao wa urefu wa kilomita 4,828, visiwa vyake vikiwa vimechangia 3.7% ya urefu huu.

Eneo la maji ya ziwa limegawanywa 6% (4,100 km2) nchini Kenya, 45% (31,000 km2) nchini Uganda, na 49% (33,700 km2) nchini Tanzania.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Watersheds of Africa: A10 Nile | Lake Victoria

Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Victoria (ziwa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.