Tunisia
Wimbo wa Taifa | Humata l-hima |
Lugha rasmi | Kiarabu |
Mji mkuu | Tunis |
Aina ya serikali | Jamhuri |
Rais | Kais Saied (قيس سعيد) |
Waziri Mkuu | Kamel Madouri (كمال المدوري) |
Eneo | km² 163.610 |
Wakazi | 11,708,370 (Julai 2020) |
Wakazi kwa km² | 71.65 |
Uhuru | 20 Machi 1956 (kutoka Ufaransa) |
Pesa | Dinari ya Tunisia |
Wakati | UTC +1 |
Sikukuu ya Taifa | 7 Novemba |
Tunisia (kirefu: Jamhuri ya Tunisia - kwa Kiarabu الجمهرية التونسية, al-Jumhūrīya at-Tūnisīya) ni nchi ya Afrika ya Kaskazini inayopakana na Bahari ya Mediteranea, Libya na Algeria.
Nchi imegawanyika katika mikoa 6 tena katika wilaya 24.
Mji mkuu ni Tunis (wakazi 1,066,961) ulioko mahali pa Karthago ya kale.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Tunisia iliwahi kutawaliwa na Wafinikia walioanzisha huko mji wa Karthago.
Baada ya hao kushindwa na Roma ya Kale, ilikuwa jimbo la Afrika katika Dola la Roma.
Kisha eneo lake likatawaliwa kwa awamu na Wavandali, Waarabu, Wahispania, Waturuki na Wafaransa.
Tarehe 20 Machi 1956 ilipata uhuru.
Watu
[hariri | hariri chanzo]Wakazi karibu wote (98%) wanajiita Waarabu na hutumia lugha ya Kiarabu ambacho ndicho lugha rasmi. Hata hivyo damu yao ni mchanganyiko hasa wa ile ya Waberber, Waarabu na Waturuki.
Takriban watu 200,000, hasa kusini, wanaendelea kuzungumza Kiberber ambacho ni lugha asili ya wenyeji lakini Waberber wengi wamezoea kutumia Kiarabu.
Katika elimu na biashara Kifaransa kinatumika pia sana.
Upande wa dini, Uislamu unafuatwa na asilimia 99 za wakazi, nao ndio dini rasmi, lakini theluthi moja kati yao, na nusu kati ya vijana, wanajitambulisha kama wasio na dini, kiwango kikubwa kuliko nchi zote za Kiarabu. Waliobaki ni Wakristo, hasa Wakatoliki, na Wayahudi wachache.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Orodha ya miji ya Tunisia
- Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
- Demografia ya Afrika
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Government of Tunisia (official website).
- Tunisia entry at The World Factbook
- Tunisia katika Open Directory Project
- Tunisia profile from BBC News.
- Wikimedia Atlas of Tunisia
Algeria | Italy Mediterranean Sea |
Italy Malta Mediterranean Sea |
||
Algeria | Mediterranean Sea | |||
Tunisia | ||||
Algeria | Algeria Libya | Libya |
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Tunisia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |