Mtakatifu Ireneo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Irenaeus, Askofu wa Lyon.

Mtakatifu Ireneo (kwa Kigiriki: Εἰρηναῖος, Eirēnaios 130 hivi – 202 hivi) alikuwa askofu wa pili wa mji wa Lyon, leo nchini Ufaransa, aliyewajibika kueneza Ukristo katika eneo hilo lote.

Zaidi ya hayo, alistawisha teolojia kwa kupinga uzushi hata kwa maandishi bora[1] ya Kigiriki, lugha mama yake.

Ametambuliwa tangu kale kuwa mtakatifu kama mfiadini. Tarehe 21 Januari 2022 Papa Fransisko alimuongezea sifa ya "mwalimu wa Kanisa" [2]

Sikukuu yake ni tarehe 28 Juni[3].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Ireneo alizaliwa yapata mwaka 130 akalelewa Kikristo katika mji wa Smirna (leo İzmir nchini Uturuki), akiwa mwanafunzi wa Mt. Polikarpo aliyekuwa askofu wa mji huo baada ya kuwa mfuasi wa Mtume Yohane.

Mwaka 177, baada ya kuhamia Ufaransa, Ireneo alipata upadrisho huko Lyons, na baada ya kutumwa kidogo Roma kama mjiumbe kwa Papa, akinusurika hivyo kuuawa katika dhuluma dhidi ya Wafiadini wa Lyon, aliteuliwa kuwa askofu wa hapo baada ya Potinus[4].

Ni muhimu kwa juhudi zake za kupigania umoja wa Kanisa dhidi ya uzushi, akisisitiza umuhimu wa mlolongo wa kitume wa maaskofu, akitoa kama mfano orodha ya wale wa Kanisa la Roma baada ya Mtume Petro. Alidai makanisa yalingane na imani ya Kanisa hilo. Hata hivyo alimsihi Papa Vikta I asiwatenga na Kanisa Wakristo wa Asia Ndogo kwa sababu tu ya tofauti za kiliturujia[5].

Katika maandishi yake alijitahidi sana kutetea imani ya Kanisa Katoliki inayotegemea mapokeo ya Mitume wa Yesu[6] dhidi ya mafundisho ya Wagnosi yaliyotegemea ujuzi ambao yeyote alidai kuwa nao akianzisha kikundi chake.

Ni wa kwanza pia kushuhudia Injili nne kuwa Neno la Mungu.

Kwa mujibu wa mapokeo, aliifia dini yake mnamo mwaka 200.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. His best-known work is Adversus Haereses, a refutation of gnosticism, in particular that of Valentinus. To counter the doctrines of the gnostic sects claiming secret wisdom, he offered three pillars of orthodoxy: the scriptures, the tradition handed down from the apostles, and the teaching of the apostles' successors. Intrinsic to his writing is that the surest source of Christian guidance is the Church of Rome, and he is the earliest surviving witness to regard all four of the now-canonical gospels as essential.
  2. http://www.causesanti.va/it/notizie/notizie-2022/decreto-del-santo-padre-per-il-conferimento-del-titolo-di-dottor.html
  3. Martyrologium Romanum
  4. Book V Chapter 4, Section 1
  5. Book V Chapter 24, Section 1ff
  6. Irenaeus cited the New Testament approximately 1,000 times. About one third of his citations are made to Paul's letters.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.