Kanuni ya Imani ya Mitume

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa karne ya 13 ukionyesha Thenashara wakiandika Kanuni ya Imani, ilivyosadikika wakati huo.


Kanuni ya Imani ya Mitume (kwa Kilatini: Symbolum Apostolorum au Symbolum Apostolicum) ni ungamo la imani ya Ukristo lililoanza kutumika mjini Roma katika karne ya 2 kwa ajili ya ubatizo, halafu likaenea hasa katika Kanisa la Magharibi.[1]

Kanuni hiyo inaendelea kutumiwa na Kanisa Katoliki na madhehebu mengi ya Uprotestanti katika liturujia na katekesi.

Kwa kuwa ilitokea Ulaya Magharibi, ambapo elekeo la kinadharia si kubwa kama huko Ugiriki, tena mapema kuliko mabishano mengi ya teolojia kuhusu umungu wa Yesu Kristo na wa Roho Mtakatifu, haina ufafanuzi wa kina.

Maandishi ya zamani zaidi tuliyonayo yanayoitaja "Kanuni ya Imani ya Mitume" ni barua ya mwaka 390 hivi kutoka sinodi ya Milano kwa Papa Siricius.[2][3][4]

Matini kwa Kilatini

Credo in Deum Patrem omnipotentem, Creatorem caeli et terrae,
et in Iesum Christum, Filium Eius unicum, Dominum nostrum,
qui conceptus est de Spiritu Sancto, natus ex Maria Virgine,
passus sub Pontio Pilato, crucifixus, mortuus, et sepultus,
descendit ad inferos, tertia die resurrexit a mortuis,
ascendit ad caelos, sedet ad dexteram Patris omnipotentis,
inde venturus est iudicare vivos et mortuos.
Credo in Spiritum Sanctum,
sanctam Ecclesiam catholicam, sanctorum communionem,
remissionem peccatorum,
carnis resurrectionem,
vitam aeternam.
Amen.[5]

Tafsiri ya Kiswahili

Imani ya Mitume (umbo la Kanisa Katoliki)[6] Imani ya Mitume (umbo la Kanisa la Kilutheri)[7]
Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, mwumba mbingu na dunia. Namwamini Mungu, BabaMwenyezi, Muumba wa mbingu na nchi.
na kwa Yesu Kristo, Mwanae pekee, Bwana wetu, aliyetungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria,

akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu


Siku ya tatu akafufuka kutoka wafu, akapaa mbinguni, ameketi kuume kwa Mungu Baba mwenyezi; kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.

Namwamini Yesu Kristo, Mwana wake wa pekee, Bwana wetu, aliyechukiliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Mariamu;

Akateswa zamani za Pontio Pilato, akasulibiwa, akafa, akazikwa, akashuka kuzimu;


Siku ya tatu akafufuka kutoka kwa wafu: Akapaa mbinguni, ameketi mkono wa kuume wa Mungu, Baba Mwenyezi. Kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.

Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu katoliki, ushirika wa watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, na uzima wa milele. Amina. Namwamini Roho Mtakatifu: Kanisa takatifu la Kikristo lililo moja tu[8]; ushirika wa watakatifu. Ondoleo la dhambi, kufufuliwa kwa mwili, na uzima wa milele. Amen.

Tanbihi

  1. Neno la Kilatini symbolum, ishara, zawadi, linatokana na Kigiriki σύμβολον, kutoka kitenzi συμβάλλειν, kuweka pamoja, kulinganisha" (The American Heritage Dictionary of the English Language).
  2. Jack Rogers, Presbyterian Creeds (Westminster John Knox Press 1985 ISBN 978-0-664-25496-4), pp. 62–63
  3. "James Orr: The Apostles' Creed, in International Standard Bible Encyclopedia". Reformed.org. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-22. Iliwekwa mnamo 2011-05-19. 
  4. "Apostles Creed". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-03-12. Iliwekwa mnamo 2014-09-21. 
  5. "Catechismus Catholicae Ecclesiae". Vatican.va. 1992-06-25. Iliwekwa mnamo 2014-08-05. 
  6. Misale ya Waamini, toleo la mwaka 2021, uk. 513
  7. Matini iliyochapishwa katika kitabu cha Tumwabudu Mungu Wetu 2012, kilichotolewa na KKKT, ISBN 9987-652-08-5
  8. Wamoravian wanasema hapa: Kanisa takatifu lililopo popote

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kanuni ya Imani ya Mitume kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.