Potinus wa Lyon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kanisa la Mt. Potinus huko Lyon.

Potinus (kwa Kifaransa Saint Pothin) alikuwa askofu wa Lyon aliyeuawa mwaka 177 wakati wa dhuluma ya kaisari Marcus Aurelius dhidi ya Ukristo.

Askofu Ireneo wa Lyon alimtaja kama mtangulizi wake katika barua ambayo anadhaniwa kuwa aliwaandikia Wakristo wa mkoa wake wa asili, Asia ndogo. Kadiri yake, Potinus alizaliwa mwaka 87 huko Frigia (katika Uturuki wa leo) akatumwa na Polikarpo wa Smirna kufanya umisionari Ulaya magharibi pamoja na Wakristo wengine.

Anahesabiwa kuwa askofu wa kwanza wa Ufaransa[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kwama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Juni[2] pamoja na wenzake 47: mtumwa bikira Blandina wa Lyon, Aleksanda, Attalus, Vezi Espagati, Maturus, shemasi Sanctius, padri Zakaria, Makari, Asklibiade, Silvio, Primo, Ulpio, Vitale, Komino, Oktoba, Filomeno, Gemino, Julia, Albina, Grata, Emilia, Potamia, Pompea, Rodana, Biblis, Kwarsya, Materna, Elpis, Pontiko, Isto, Aristeo, Korneli, Zosimo, Tito, Julius, Zotiko, Apoloni, JeminianI, Julia mwingine, Ausona, Emilia mwingine, Iamnika, Pompea mwingine, Domna, Yusta, Trofima na Antonia.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.