Blandina wa Lyon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya Mt. Blandina.
Fresque de la chapelle orthodoxe de la Dormition de la Mère de Dieu (Drôme).

Blandina (kwa Kifaransa: Blandine; alifariki Lyon, leo nchini Ufaransa, 177) alikuwa mwanamke mtumwa aliyeuawa katika dhuluma wa kaisari Marcus Aurelius dhidi ya Wakristo[1].

Barua iliyotufikia kutoka kwa walionusurika kuuawa wakati huo inaleta ripoti kali lakini sahihi ya mauaji hayo ya wafiadini wa Lyon yaliyofanyika katika mji mkuu wa Gallia.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu bikira na mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Juni[2] pamoja na wenzake 47: askofu Potinus wa Lyon, Aleksanda, Attalus, Vezi Espagati, Maturus, shemasi Sanctius, padri Zakaria, Makari, Asklibiade, Silvio, Primo, Ulpio, Vitale, Komino, Oktoba, Filomeno, Gemino, Julia, Albina, Grata, Emilia, Potamia, Pompea, Rodana, Biblis, Kwarsya, Materna, Elpis, Pontiko, Isto, Aristeo, Korneli, Zosimo, Tito, Julius, Zotiko, Apoloni, JeminianI, Julia mwingine, Ausona, Emilia mwingine, Iamnika, Pompea mwingine, Domna, Yusta, Trofima na Antonia.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.