Wafiadini wa Lyon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kiwanja cha michezo cha Lyon kikiwa na mahali pa kuheshimu wafiadini waliouawa humo.

Wafiadini wa Lyon ndio Wakristo wafiadini wa kwanza wa Ufaransa[1].

Ni kwamba mwaka 177 dhuluma ya kaisari Marcus Aurelius dhidi ya Ukristo ilisababisha mauaji makubwa katika mji mkuu wa Gallia, jina lake Lugdunum (siku hizi Lyon).

Kati yao, ni maarufu hasa askofu Potinus wa Lyon na mtumwa bikira Blandina wa Lyon. Wengine ni: Aleksanda, Attalus, Vezi Espagati, Maturus, shemasi Sanctius, padri Zakaria, Makari, Asklibiade, Silvio, Primo, Ulpio, Vitale, Komino, Oktoba, Filomeno, Gemino, Julia, Albina, Grata, Emilia, Potamia, Pompea, Rodana, Biblis, Kwarsya, Materna, Elpis, Pontiko, Isto, Aristeo, Korneli, Zosimo, Tito, Julius, Zotiko, Apoloni, JeminianI, Julia mwingine, Ausona, Emilia mwingine, Iamnika, Pompea mwingine, Domna, Yusta, Trofima na Antonia.

Nusu walikuwa wenyeji, nusu walowezi kutoka Frigia, leo nchini Uturuki.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 2 Juni[2].

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/60450
  2. Martyrologium Romanum