Nenda kwa yaliyomo

Ufini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Finlandi)
Suomen tasavalta
Republiken Finland

Jamhuri ya Ufini
Bendera ya Ufini Nembo ya Ufini
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: none
Wimbo wa taifa: Maamme (Kifini)
Vårt land (Kiswidi)
("Nchi yetu" Kiswahili)
Lokeshen ya Ufini
Mji mkuu Helsinki
60°10′ N 24°56′ E
Mji mkubwa nchini Helsinki
Lugha rasmi Kifini (89.33%), Kiswidi (5.34%)
Serikali Jamhuri2
Alexander Stubb
Petteri Orpo
Uhuru
imetangazwa
6 Desemba 1917
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
338,145 km² (ya 64)
9.4
Idadi ya watu
 - 2014 kadirio
 - 2000 sensa
 - Msongamano wa watu
 
5,470,820 (ya 115)
5,181,115
16/km² (ya 201)
Fedha Euro (€)1 (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
EET (UTC+2)
EEST (UTC+3)
Intaneti TLD [.fi]
Kodi ya simu +358

-

1Prior to 1999: Finnish markka
2Semi-presidential system


Pielinen

Ufini (kwa Kifini: Suomi) ni nchi ya Skandinavia iliyoko Ulaya ya Kaskazini. Imepakana na Norwei upande wa kaskazini, Urusi upande wa mashariki na Uswidi upande wa magharibi. Ng'ambo ya Baltiki iko Estonia ambayo watu wake hutumia lugha iliyo karibu sana na Kifini. Inaonekana ya kwamba mababu wa Wafini na Waestonia walihama pamoja wakiwa na lugha ileile zamani, lakini sasa ni lugha mbili kwa sababu hawakuwa na mawasiliano kati yao kwa muda mrefu.

Nchi ina wakazi milioni tano unusu tu katika eneo la km² 338,000; hivyo ni kati ya nchi za Ulaya zenye msongamano mdogo wa watu. Sehemu kubwa ya eneo lake ni misitu tu. Mji mkuu ni Helsinki; mji muhimu mwingine ni Tampere, mji ulioko karibu kilomita 180 kaskazini mwa Helsinki, ni wa pili kwa ukubwa. Miji mingine mikubwa ni pamoja na Turku, Kuopio na Vaasa.

Ufini ilijitegemea mnamo 1917. Kati ya 1939 na 1944, Ufini ilipigana dhidi ya Umoja wa Kisovyeti na jeshi la Ufini liliongozwa na kamanda Carl Gustaf Emil Mannerheim.

Nchi ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa na wa Umoja wa Ulaya.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Historia ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Ufini ulikaliwa na watu tangu ilipokwisha enzi ya barafu ya mwisho, miaka 9000 KK hivi.[1] Wakazi wa kwanza walikuwa wawindaji-wakusanyaji ambao walitumia vifaa vya mawe vinavyofanana na vile vya Estonia, Russia na Norway.

Labda kilimo kilianza miaka 3000 KK - 2500 KK.[2]

Mwishoni mwa karne ya 13 Ufini ukawa sehemu ya Sweden hadi mwaka 1809, ilipomezwa na Urusi kama ufalme mdogo wenye kujitawala kwa kiasi fulani.

Karne ya 20

[hariri | hariri chanzo]
Carl Gustaf Emil Mannerheim

Mwaka 1906, Ufini ulikuwa nchi ya kwanza duniani kuwapa wananchi wote wenye umri wa utu uzima haki ya kugombea vyeo vya serikali.[3][4]

Mwaka 1917, baada ya Mapinduzi ya Russia, Ufini ulijitangaza huru na mwaka uliofuata ukawa jamhuri baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Wakati wa vita vikuu vya pili, Muungano wa Kisovyeti ulijitahidi kuteka Ufini wote, ukaishia kutwaa Karelia, Salla, Kuusamo, Petsamo na visiwa kadhaa tu.

Baada ya vita Ufini uliacha kutegemea kilimo ukajitosa katika uchumi wa viwanda[5] hata kufikia kuwa kati ya nchi zilizoendelea zaidi[6][7][8][9][10][11][12].

Mwaka 1955 Ufini ulijiunga na Umoja wa Mataifa ukichagua siasa ya kutoambatana na upande wowote.

Mwaka 1995 ulijiunga na Umoja wa Ulaya na mwaka 1999 ulikubali kutumia euro.

Ufini inajulikana kama "Nchi ya Maziwa Maelfu".[13]

Kuna jumuiya tatu katika Ufini:

  • Wafini wenyewe ambao ni 90% ya wakazi wote.
  • Waswidi wako hasa upande wa kusini mwa nchi, kwa jumla ni takriban 5% ya wakazi; hasa visiwa vya Aland kuna Waswidi watupu walio na hali ya kujitawala ndani ya Ufini.
  • Wakazi asilia ni Wasami ambao wako kaskazini tu. Maisha yao yanategemea uwindaji na ufugaji; wako wachache, jumla yao haifikii 0.2% ya wakazi wote.

Mbali na hao, kuna wahamiaji (5.9%), hasa kutoka Russia, Estonia na Somalia.

Lugha rasmi ni Kifini na Kiswidi. Lugha ya Kifini ina asili ya Asia ya Kati, haina uhusiano na lugha za Kihindi-Kiulaya.

Wakazi wenye lugha ya Kiswidi wako upande wa kusini mwa nchi kwa sababu Ufini ilitawaliwa na Uswidi kwa karne nyingi. Katika karne hizo walikuwepo Waswidi waliohamia Ufini lakini kuna pia Wafini walioanza kutumia Kiswidi pekee. Hasa kwenye visiwa vya Aland Kiswidi ni lugha pekee. Lakini Waswidi wa Ufini wanajisikia wa Ufini.

Upande wa dini, 72% ni Walutheri na 1.1% Waorthodoksi. Madhehebu hayo mawili ya Ukristo yanatambulika na kupewa nafasi katika matukio mbalimbali na shuleni. 1,6% wanafuata dini au madhehebu mengine, wakati 25.3% hawana dini yoyote.

Watu maarufu

[hariri | hariri chanzo]
  • Mikael Agricola
  • Urho Kaleva Kekkonen
  • Elias Lönrrot
  • Garlf Gustaf Emil Mannerheim
  • Martti Ahtisaari
  • Alvar Aalto
  • Jean Sibelius

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Georg Haggren, Petri Halinen, Mika Lavento, Sami Raninen and Anna Wessman (2015). Muinaisuutemme jäljet. Helsinki: Gaudeamus. uk. 23. ISBN 978-952-495-363-4.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  2. Georg Haggren, Petri Halinen, Mika Lavento, Sami Raninen ja Anna Wessman (2015). Muinaisuutemme jäljet. Helsinki: Gaudeamus. uk. 339. ISBN 9789524953634.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  3. Parliament of Finland. "History of the Finnish Parliament". eduskunta.fi. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-09-26. Iliwekwa mnamo 2018-02-20.
  4. Finland was the first nation in the world to give all (adult) citizens full suffrage, in other words the right to vote and to run for office, in 1906. New Zealand was the first country in the world to grant all (adult) citizens the right to vote, in 1893. But women did not get the right to run for the New Zealand legislature, until 1919.
  5. "Finland". International Monetary Fund. Iliwekwa mnamo 17 Aprili 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Finland: World Audit Democracy Profile". WorldAudit.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Oktoba 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Tertiary education graduation rates—Education: Key Tables from OECD". OECD iLibrary. 14 Juni 2010. doi:10.1787/20755120-table1. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-04-30. Iliwekwa mnamo 6 Machi 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. "Her er verdens mest konkurransedyktige land—Makro og politikk". E24.no. 9 Septemba 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Oktoba 2010. Iliwekwa mnamo 6 Machi 2011. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
  9. "The 2009 Legatum Prosperity Index". Prosperity.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Oktoba 2009. Iliwekwa mnamo 4 Februari 2010. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "Human Capital Report 2015". World Economic Forum. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-12-03. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. "Fragile States Index 2016". Fundforpeace.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Februari 2017. Iliwekwa mnamo 27 Novemba 2016. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
  12. Gender Gap Report (PDF). WEF.
  13. Li, Leslie (1989-04-16). "A Land of a Thousand Lakes". The New York Times (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-12-29.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ufini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.