Malta
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: -- | |||||
Wimbo wa taifa: L-Innu Malti | |||||
Mji mkuu | Valletta | ||||
Mji mkubwa nchini | Birkirkara | ||||
Lugha rasmi | Kimalta, Kiingereza | ||||
Serikali | Jamhuri George Vella Robert Abela | ||||
Uhuru Kutoka Uingereza Jamhuri |
21 Septemba 1964 13 Desemba 1974 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
316 km² (ya 185) 0.001 | ||||
Idadi ya watu - 31 Machi 2013 kadirio - 2011 sensa - Msongamano wa watu |
446,547 (ya 171) 416,055¹ 1,562/km² (ya 7) | ||||
Fedha | Lira ya Malta (Lm) (Euro kuanzia Januari 2008) ( MTL )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) | ||||
Intaneti TLD | .mt 2 | ||||
Kodi ya simu | +356
- |
Malta ni nchi ndogo kwenye funguvisiwa katikati ya bahari ya Mediteranea.
Malta iko km 93 kusini kwa kisiwa cha Sisilia (Italia), upande wa mashariki kwa Tunisia na kaskazini kwa Libya.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Funguvisiwa la Malta lina visiwa saba. Visiwa vikubwa viwili ni Malta (km² 246) na Gozo (km² 70). Kuna kisiwa cha tatu kinachokaliwa na watu, ndicho Comino (km² 3). Vingine ni vidogo, havina watu. Jumla la eneo ni km² 316.
Visiwa vya Malta ni mabaki ya kanda la nchi kavu lililokuwa linaunganisha Afrika na Ulaya na lililokatwa na kupanda kwa usawa wa bahari tangu mwaka 11000 KK hivi.
Sehemu za juu ni vilima vya Dingli Cliffs vyenye kimo cha mita 245 juu ya UB.
Tatizo kubwa la Malta ni uhaba wa maji baridi. Siku hizi vituo vinne vya kuondoa chumvi kwenye maji ya bahari kwa njia ya osmosi vinatengeneza maji ya kunywa. Maji machafu husafishwa na mvua kukusanywa.
Miji
[hariri | hariri chanzo]Miji mikubwa zaidi ni: St. Paul's Bay (29,097), Birkirkara (wakazi 21,676), Qormi (wakazi 18,230), Mosta (wakazi 17,789), Zabbar (wakazi 15,030), Victoria (wakazi 12,914) na San Gwann (wakazi 12,346).
Mji mkuu, Valletta, una wakazi 7,173 tu.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Malta ilikaliwa na watu tangu milenia ya 4 KK. Kuna magofu ya hekalu la mwaka 3200 KK hivi.
Baadaye funguvisiwa lilitawaliwa na Wafinisia, Karthago na Dola la Roma.
Malta inatajwa katika Biblia kwa sababu Mtume Paulo aliponea huko baada ya kuzama kwa merikebu alimosafiri baharini kuelekea Roma (Mdo 27:39 n.k.).
Waarabu walivamia visiwa hivyo mwaka 870 na kuvitawala hadi 1091.
Baadaye vilitawaliwa na Wanormandi wa Italia Kusini, halafu na Wahispania chini ya mamlaka ya Dola Takatifu la Kiroma la Ujerumani.
Tangu mwaka 1530 visiwa vilikabidhiwa na Kaisari kwa askari wa Vita vya msalaba wa Chama cha Wanahospitali wa Mt. Yohane wa Yerusalemu.
Wanamisalaba hao walitawala visiwa hivyo hadi Napoleoni alipoteka Malta mwaka 1799 akiwa safarini kwenda Misri.
Uingereza ulitwaa visiwa kutoka kwa Ufaransa ukatawala Malta hadi uhuru wake tarehe 21 Septemba 1964.
Tarehe 13 Desemba 1974 Malta ikatangazwa kuwa jamhuri ndani ya Jumuiya ya Madola.
Tarehe 1 Mei 2004 nchi ikajiunga na Umoja wa Ulaya.
Watu
[hariri | hariri chanzo]Kwa jumla kuna wakazi 404,039: wa kiume 200,715 (49.7%) na wa kike 203,324 (50.3%). Msongamano wa watu ni 1,282 kwa kilomita ya mraba ambao ni msongamano mkubwa kati ya nchi zote za Ulaya. Katika karne ya 21 nchi imepokwa wahamiaji wengi, ambao kwa sasa ni 23.17% za wakazi wote.
Lugha ya Kimalta ni lugha ya pekee. Asili yake ni lahaja ya Kiarabu iliyopokea maneno mengi ya Kiitalia, Kisisili, Kiingereza, Kihispania na Kifaransa. Ni lugha pekee ya Kisemiti inayoandikwa rasmi kwa alfabeti ya Kilatini.
Lugha rasmi ya pili ni Kiingereza kutokana na miaka 150 ya ukoloni wa Uingereza. Wamalta wengi sana (66%) huelewa pia lugha ya nchi kubwa jirani, Italia.
wakazi wengi (90%) ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (83%), ambalo imani yake ndiyo dini rasmi ya nchi. Waislamu ni asilimia 2.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Cramer, John Anthony (1828). Geographical and Historical Description of Ancient Greece. Clarendon Press. ku. 45–46.
- "Map of Malta and Gozo". Street Map of Malta and Gozo. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-16. Iliwekwa mnamo 10 Aprili 2009.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - "Photos of Gozo sister island of Malta". Photos of Gozo. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-10-23. Iliwekwa mnamo 17 Novemba 2006.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - "Photos of Malta". Photos of Malta. Iliwekwa mnamo 26 Mei 2008.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - "Malta". CIA World Factbook. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-10-16. Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2006.
{{cite web}}
: Unknown parameter|=
ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - "Gov.mt". Government of Malta. Iliwekwa mnamo 1 Novemba 2005.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - "Malta". Malta. http://encarta.msn.com/encyclopedia_761555566/Malta.html. Retrieved 1 November 2005. Archived 28 Oktoba 2009 at the Wayback Machine.
- "1942: Malta gets George Cross for bravery", BBC "On this day", 15 April 1942. Retrieved on 22 June 2006.
- Jones, H. Bowen; na wenz. (1962). Malta Background for Development. Dhurham College. OCLC 204863.
{{cite book}}
: Explicit use of et al. in:|author2=
(help) - Carolyn Bain (2004). Malta. Lonely Planet Publication. ISBN 1-74059-178-X.
- Paul Williams (2009). Malta – Island Under Siege. Pen and Sword Books. ISBN 978-1-84884-012-6. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-04-05. Iliwekwa mnamo 2014-11-11.
{{cite book}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - Charles Mifsud, The Climatological History of The Maltese Islands, Minerva 1984
- Rudolf, Uwe Jens; Berg, W. G. (2010). Historical Dictionary of Malta. USA: Scarecrow Press. uk. 43. ISBN 9780810853171.
- United Nations Development Programme (2006). Human Development Report 2005 – International cooperation at a crossroads: Aid, trade and security in an unequal world. Oxford University Press. ISBN 0-19-522146-X.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]
- Serikali
- Tovuti rasmi
- Laws of Malta The Official Laws of Malta website
- The Maltese Armed Forces official website Archived 15 Aprili 2012 at the Wayback Machine.
- Malta Environment and Planning Authority's Archived 8 Desemba 2008 at the Wayback Machine. GIS
- FinanceMalta official website Archived 28 Januari 2013 at the Wayback Machine.
- Taarifa za jumla
- Malta Archived 24 Novemba 2020 at the Wayback Machine. – Wiki about Malta containing both general and travel related information
- Malta entry at The World Factbook
- Malta Archived 15 Oktoba 2008 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Malta katika Open Directory Project
- Malta profile from the BBC News
- Wikimedia Atlas of Malta
- Migration Malta Archived 6 Aprili 2011 at the Wayback Machine. – An information source on immigration and Malta (scholarly articles, policy documents, press releases etc.)
- Vyombo vya habari
- MaltaMedia Archived 9 Oktoba 2020 at the Wayback Machine. – online news
- The Times of Malta
- Malta Film Commission
- Bartolomy's photos of Malta January 2014 Archived 26 Machi 2015 at the Wayback Machine.
- Safari
- Official Maltese Tourism website
- Valletta Living History Official Website
- Photos, Webcam of Gozo Archived 23 Oktoba 2008 at the Wayback Machine.
Nchi za Umoja wa Ulaya | |
---|---|
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Malta kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |