Valletta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kitovu cha kihistoria cha Valetta
Valetta mnamo 1680 kwa macho ya ndege

Valetta (pia: La Valetta, Kilugha: il-belt "mji") ni mji mkuu wa Malta mwenye wakazi 7,100. Mji ulijengwa kama mji-boma kwenye ncha ya rasi ndogo inayozungukwa na maji ya bahari pande tatu.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Valetta limepokea jina lake kwa heshima ya Jean de la Valette aliyekuwa mkuu wa wamisalaba wa chama cha hospitali ya Mt. Yohane wa Yerusalemu. Valette aliamuru kujengwa kwa mji huu baada ya uvamizi wa Waturuki waliojaribu kuteka Malta mwaka 1565. Waturuki hawakufaulu wakafukuzwa na Valette aliona haja ya kuwa na mji imara kabisa kama wanataka kurudi. Hivyo mji mpya ulijengwa kuanzia mwaka 1566 kwenye ncha ya rasi penye bandari asilia bora.

Mnamo mwaka 1700 Valetta ilikuwa mji mwenye ukuta imara kushinda miji yote.

Mji una majengo mengi ya kihistoria ukaingizwa katika orodha ya UNESCO ya urithi wa dunia.

Idadi ya wakazi imepungua kwa sababu watu wengi walijenga mashambani.

Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Valletta kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.