Nenda kwa yaliyomo

Timor ya Mashariki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Timor Mashariki)
Repúblika Demokrátika Timor Lorosa'e
República Democrática de Timor-Leste

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Timor ya Mashariki
Bendera ya Timor ya Mashariki Nembo ya Timor ya Mashariki
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: "Honra, Pátria e Povo"  (Kireno)
"Heshima, Taifa na Watu"
Wimbo wa taifa: Pátria
Lokeshen ya Timor ya Mashariki
Mji mkuu Dili
8°34′ S 125°34′ E
Mji mkubwa nchini Dili
Lugha rasmi Kitetum, Kireno1
Serikali Jamhuri
José Ramos-Horta
Taur Matan Ruak
Uhuru
Ilitangazwa
Ilikubaliwa
{{{established_dates}}}
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
15,007 km² (ya 159)
kidogo sana
Idadi ya watu
 - Julai 2021 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
1,340,513 (ya 153)
78/km² (ya 137)
Fedha U.S. Dollar3 (USD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+9)
(UTC)
Intaneti TLD .tl3
Kodi ya simu +670

-

1 Kiingereza na Kiindonesia vimekubaliwa na katika ya nchi kama "lugha za kazi".
2 Indonesia ilivamia Timor tar. 7 Desemba 1975 na kuondoka 1999.
3 Kuna pia sarafu za centavo ya Timors ya Mashariki.Ramani

Timor ya Mashariki (kwa Kireno Timor-Leste, kwa Kitetum Timór Lorosa'e; jina rasmiː República Democrática de Timor-Leste au Repúblika Demokrátika Timór-Leste) ni nchi ya Asia ya kusini-mashariki kwenye kisiwa cha Timor, takriban km 640 kaskazini kwa Darwin, Australia.

Eneo lake ni nusu ya mashariki ya kisiwa hicho pamoja na visiwa vya Atauro na Jaco. Kuna pia eneo dogo upande wa magharibi ya Timor ambao kwa kiasi kikubwa uko chini ya Indonesia pamoja na visiwa vya jirani.

Eneo lote la nchi ni km² 15,007.

Mji mkuu ni Dili wenye wakazi 245,000.

Timor ya Mashariki ni kati ya nchi maskini zaidi duniani.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Wakazi ni mchanganyiko wa Wapapua-Wamelanesia waliofika miaka 40,000 iliyopita, Waaustronesia waliofika kama mwaka 3000 KK na Wamalay waliokuwa wa mwisho.

Timor ilikuwa kituo cha biashara cha Wareno tangu karne ya 16. Maeneo mengine ya visiwa vya Indonesia ya leo yalivamiwa na Waholanzi na Timor ilibaki kisiwa pekee chini ya utawala wa Ureno katika sehemu hii ya dunia.

Katika karne ya 19 Waholanzi walifika pia Timor. Mikataba ya 1859 na 1916 zilithibitihsa ugawaji wa kisiwa. Sehemu ya magharibi ilikuwa chini ya Uholanzi na baadaye sehemu ya Indonesia, lakini sehemu ya mashariki ilibaki koloni la Ureno.

Baada ya mapinduzi ya Ureno ya 1974 Wareno waliondoka Timor bila maandalizi na kutosha. Viongozi wazalendo walitangaza uhuru. Lakini siku chache baada ya tangazo hilo, jeshi la Indonesia lilivamia nchi ambayo ikatangazwa kuwa jimbo la Indonesia. Hali hii haikutambuliwa na Umoja wa Mataifa.

Vita vikali vya msituni vilifuata kati ya wapigania uhuru na jeshi la Indonesia.

Mabadiliko yalipatikana mwaka 1998 baada ya rais Suharto wa Indonesia kujiuzulu, na rais mpya Bacharuddin Jusuf Habibie kuwa tayari kuipa Timor ya Mashariki hali ya kujitawala ndani ya Indonesia.

Karibu wananchi wote (98 %) walihudhuria katika kura ya maoni ya tarehe 30 Agosti 1999 na zaidi ya robo tatu (78,5 %) walipigia kura uhuru badala ya kuwa jimbo la kujitawala.

Baada ya kura hii jeshi la Indonesia lililipiza kisasi kwa kuua watu wengi na kuharibu nyumba lakini macho ya dunia yalitazama Timor, na serikali ya Indonesia kwa tishio la kufutiwa mikopo ya benki ya dunia ililazimishwa kuondoa jeshi lake na kukubali kufika kwa jeshi la Umoja wa Mataifa chini ya uongozi wa Australia.

Tangu tarehe 27 Septemba 2002 Timor ya Mashariki ni nchi mwanachama wa UM.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Kuna lugha 19 ambazo huzungumzwa nchini Timor ya Mashariki. Lugha rasmi ni Kitetum (lugha mama ya 30.6% za wakazi), ambacho ni kati ya lugha za Austronesia, pamoja na Kireno.

Upande wa dini, wananchi karibu wote (99.53%) ni wafuasi wa Yesu Kristo katika Kanisa Katoliki (97.57%) na madhehebu ya Uprotestanti (1.96%). Wengi walijiunga na Kanisa wakati wa vita vya ukombozi. Waislamu ni 0.24%.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Taarifa za jumla
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Timor ya Mashariki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.