Mkopo (fedha)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkopo


Mkopo (kutoka kitenzi "kukopa"; kwa Kiingereza: "loan") wa kifedha ni pesa ambazo mtu au shirika anapewa na benki, asasi ya fedha ya ushirika (SACCOS)[1], kundi au mashirika mengine yaliyoidhinishwa kufanya biashara ya fedha. Anayepata mkopo huwa na deni analofaa kulipa kulingana na makubaliano rasmi yake na anayemkopesha. Deni hili linaweza kuwa karadha[2] au mkopo unaolipwa pamoja na riba[3]. Riba ndiyo faida ya mashirika kama benki yanayofanya biashara ya ukopeshaji.

Aina za mikopo[hariri | hariri chanzo]

Kuna aina nyingi za mikopo kulingana na yanayohitajika kupata ule mkopo, anayelengwa na ule mkopo au lengo la matumizi ya ule mkopo. Mkopo unaweza kuwa fungika - mkopo unaochukuliwa kisha kulipwa kabla ya mtu kuidhinishwa mkopo mwingine - au mkopo endelevu - mkopo unaoweza kuchukuliwa mmoja baada ya mwingine bila hasa kukamilisha kulipa mkopo uliotangulia kama vile mkopo wa kadi ya mkopo (credit card)[4].

Aina za mikopo kulingana na yanayohitajika[hariri | hariri chanzo]

 • Mkopo wa dhamana - ni mkopo unaohitaji anayekopa kuwa na rasilimali kama dhamana ya mkopo, k.v. mkopo kutoka kwa benki na asasi ya fedha ya ushirika (SACCO).
 • Mkopo usio na dhama - ni mkopo usiohitaji anayekopa kuwa na rasilimali ama dhamana ya mkopo, k.v. mkopo kutoka kwa marafiki na jamii.

Aina za mikopo kulingana na lengo la matumizi[hariri | hariri chanzo]

Mashirika tofauti pia hutoa mikopo ya kazi tofautitofauti ikiwemo:

 • Mkopo wa kilimo
 • Mkopo wa biashara
 • Mkopo wa masomo
 • Mkopo wa gari
 • Mkopo wa nyumba - mikopo inayotolewa ya kununua nyumba hasa katika nchi ambazo biashara ya uuzaji wa nyumba imenawili kama vile Marekani. Nchi nyingine kuna pia mikopo ya kurekebisha na kukarabati nyumba kama vile Singapore[5].
 • Mkopo wa ardhi na rasilimali nyingine
 • Mkopo wa matumizi ya binafsi
 • Mkopo wa kulipa mikopo mingine (ujulikanao kwa Kiingereza kama consolidation loan)
 • Mkopo wa siku mbaya (ujulikanao kwa Kiingereza kama payday loans) - huu ni mkopo wa hapo kwa papo wakati mtu anahitaji pesa za dharura.

Aina za mikopo kulingana na mlengwa[hariri | hariri chanzo]

Mashirika yanayofanya biashara ya pesa na idara tofauti za serikali pia yana mikopo inayolenga kundi fulani la watu. Hii ni mikopo kama vile:

Aina ya mkopo kulingana na riba inayotozwa[hariri | hariri chanzo]

 • Mkopo uliopunguzwa riba (hujulikana kwa Kiingereza kama subsidized loans) - aina hii ya mkopo hutozwa riba ya chini, kama vile mkopo wa masomo.

Kulipa mikopo[hariri | hariri chanzo]

Mkopo ni deni linalofaa kulipwa kulingana na mkataba kati ya anayekopa na anyekopesha. Ikiwa ni mkopo karadha aliyekopa hulipa tu pesa alizokopa ilhali katika mkopo wa riba aliyekopa hulipa mtaji na riba juu yake. Malipo yanaweza kufanyika kidogo kidogo kila siku, wiki au mwezi.

Watu wengi hujikuta kwenye shida za kulipa mikopo na hupoteza mali yao kwa mawakala wa mikopo. Hivyo ni vyema mtu kukopa kwa busara na kutumia mkopo vyema. Kuna mashirika tofauti ambayo huwasaidia watu kutumia na kulipa mikopo[6] yao kwa busara.

Unyanyasaji katika mikopo[hariri | hariri chanzo]

Kupeana mikopo kwa minajili isiyo nzuri kama vile kuwapa kwa riba kubwa ambayo wajua vizuri itawafinyilia ni aina mojawapo ya unyanyasaji katika mikopo. Vilevile katika kupeana mikopo, kama hamna mamlaka ambayo inadhibiti na kuona kuwa mkopo wenyewe umetolewa kwa riba fulani, basi huo ni unyanyasaji. Mifano ni payday loans, shylocks na subprime mortage lending.

Kuna vilevile wale ambao huweka riba iwe juu sana kwa sababu anayekopa ana shida anayotaka kutatua papo hapo. Hii huitwa kwa Kiingereza "usury".

Wanaokopa pia huenda wakanyanyasa waliowakopea kwa kutolipa deni lao una kuchelewesha ulipaji.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

 1. Lunyeka, Saulo P.; Nzuki, Margreth P.; Hassan, Abdallah K. (April, 2005). Uploaded by Fpct Shelui. "Mwongozo wa Mafunzo ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo, Elimu ya Ujasiriamali na Stadi za Biashara Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii" (PDF). Mwongozo wa Mafunzo ya SACCOS (kwa Kiswahili) (Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii): 1. ISBN 978 - 9987 - 770 - 03 - 8. Iliwekwa mnamo 2018-10-15 – kutoka Academia.  Check date values in: |date= (help)
 2. eLimu. "Msamiati: Malipo". learn.e-limu.org (kwa Kiingereza). eLimu eLearning Company Limited. Iliwekwa mnamo 2018-10-15. 
 3. Paneli la Kiswahili. "Msamiati wa Malipo". swa.gafkosoft.com (kwa Kiswahili). Gafkosoft. Iliwekwa mnamo 2018-10-15. 
 4. America's Debt Help Organization. "Types of Consumer Credit & Loans". Debt.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-10-15. 
 5. Katong Credit. "Here’s Everything You Need to Know about a Singapore Renovation Loan in 2018". Katong Credit website (kwa en-US). Katong Credit Pte Ltd. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-12-27. Iliwekwa mnamo 2018-10-15. 
 6. "How to get a loan". Loan (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-12-28. 

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkopo (fedha) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.