Guinea
Jamhuri ya Gine | |
---|---|
République de Guinée (Kifaransa) Hawtaandi Gine (Kipular) ߖߌ߬ߣߍ߫ ߞߊ ߝߊߛߏߖߊߡߊߣߊ (Kimaninka) | |
Kaulimbiu ya taifa: Travail, Justice, Solidarité (Kifaransa) "Kazi, Haki, Mshikamano" | |
Wimbo wa taifa: Liberté (Kifaransa) "Uhuru" | |
Mahali pa Guinea | |
Ramani ya Guinea | |
Mji mkuu na mkubwa nchini | Conakry |
Lugha rasmi | Kifaransa |
Gine (pia: Gini; kwa Kifaransa: Guinée; kwa Kiingereza: Guinea; jina rasmi Jamhuri ya Gine) ni nchi katika Afrika ya Magharibi. Pengine inatajwa kama Gine-Conakry ili kuitofautisha na nchi za Gine-Bisau na Gine ya Ikweta.
Imepakana na Gine-Bisau, Senegal na Mali upande wa kaskazini, Kodivaa, Liberia na Sierra Leone kusini halafu Bahari ya Atlantiki upande wa magharibi.
Eneo lake ni chanzo ya mito mikubwa ya Niger, Senegal na Gambia.
Jina
[hariri | hariri chanzo]Jina la "Gine" liliwahi kutaja sehemu kubwa ya Afrika ya Magharibi kati ya jangwa la Sahara na Ghuba ya Gine ya Atlantiki likimaanisha "nchi ya watu weusi" kwa lugha ya Kiberberi.
Watu
[hariri | hariri chanzo]Makabila yaliyopo nchini ni 24. Kubwa zaidi ni lile la Wafulani (40%).
Lugha rasmi ni Kifaransa, lakini wakazi wanatumia zaidi lugha asilia kadiri ya makabila, hasa Kipular, Kimandinka, Kisusu, Kikisi, Kikpelle na Kiloma,
Upande wa dini, 85% ni Waislamu (hasa Wasuni), 8% ni Wakristo (hasa Wakatoliki) na 7% ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Ramani ya Guinea
-
Sokwe wa Bossou
-
Plage sur les Ile de Loos
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Orodha ya lugha za Guinea
- Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
- Demografia ya Afrika
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Serikali
[hariri | hariri chanzo]- (Kifaransa) Serikali ya Guinea Ilihifadhiwa 6 Januari 2010 kwenye Wayback Machine.
- (Kifaransa) Permanent UN Mission of the Republic of Guinea Ilihifadhiwa 17 Desemba 2007 kwenye Wayback Machine.
Habari
[hariri | hariri chanzo]- (Kiingereza) CIA World Factbook - Guinea Ilihifadhiwa 15 Juni 2006 kwenye Wayback Machine.
- (Kiingereza) BBC News Country Profile - Guinea
Muziki
[hariri | hariri chanzo]- Cora Connection Ilihifadhiwa 10 Oktoba 1999 kwenye Wayback Machine. West African music resources
Orodha
[hariri | hariri chanzo]- Open Directory Project - Guinea Ilihifadhiwa 25 Desemba 2005 kwenye Wayback Machine. directory category
- Stanford University - Africa South of the Sahara: Guinea directory category
- The Index on Africa - Guinea Ilihifadhiwa 24 Agosti 2004 kwenye Wayback Machine. directory category
- University of Pennsylvania - African Studies Center: Guinea directory category
- Yahoo! - Guinea Ilihifadhiwa 12 Machi 2007 kwenye Wayback Machine. directory category
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Guinea kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |