Conakry

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Jiji la Conakry
Nchi Guinea
Conakry katika Guinea

Conakry (pia: Konakry) ina wakazi 2,000,000 (mwaka 2002) ni mji mkuu wa Guinea. Mji una bandari mwambaoni wa Ghuba ya Guinea ya Atlantiki.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Chanzo cha Conakry ni kwenye kisiwa cha Tombo kilicho karibu sana na rasi ya Kaloum. Mji ulianzishwa baada ya kisiwa kuhamishwa kutoka utawala wa Uingereza chini ya Ufaransa. Wafaransa waliunganisha mwaka 1887 vijiji vinne vya Conakry, Boulbinet, Krutown na Tombo. Mwaka 1889 Conakry ilikuwa makao makuu ya utawala wa koloni ya « Mito ya Kusini (Rivières du Sud) » na tangu 1891 ya Guinea ya Kifaransa ikakua kwa sababu ya bandari yake hasa baada ya kujengwa kwa reli kwenda Kankan.

Conakry leo[hariri | hariri chanzo]

Leo kisiwa cha Tumbo kimeunganishwa na rasi ya Kaloum kwa barabara. Mji umeenea kufunika rasi yote. Kuna beledi tano mjini ambayo ni Kaloum (kitovu cha mji), Dixinn (penye chuo kikuu na balozi nyingi), Ratoma (penye vilabu na mabaa), Matam na Matoto penye uwanja wa ndege wa Gbessia.

Mahali pa kuangalia ni makumbusho ya kitaifa, masoko, jengo la Jumba la Watu, msikiti mkuu na visiwa vya Los.

Jumba la Watu katika Conakry