Nenda kwa yaliyomo

Sierra Leone

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Siera Leoni)
Republic of Sierra Leone
Bendera ya Sierra Leone Nembo ya Sierra Leone
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Unity - Freedom - Justice (Umoja, Uhuru, Haki)
Wimbo wa taifa: High We Exalt Thee, Realm of the Free (Twakusifu nchi ya watu huru)
Lokeshen ya Sierra Leone
Mji mkuu Freetown
8°31′ N 13°15′ W
Mji mkubwa nchini Freetown
Lugha rasmi Kiingereza
Serikali Jamhuri
Julius Maada Bio
Uhuru
kutoka Uingereza
27 Aprili 1961
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
71,740 km² (ya 119)
1.1
Idadi ya watu
 - Julai 2023 kadirio
 - 2000 sensa
 - Msongamano wa watu
 
8,909,040 (ya 100 1)
5,426,618
112/km² (ya 114 1)
Fedha Leone (SLL)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
GMT (UTC+0)
(UTC)
Intaneti TLD .sl
Kodi ya simu +232

-



Sierra Leone ni nchi ya Afrika ya Magharibi.

Imepakana na Guinea na Liberia, upande wa magharibi iko bahari ya Atlantiki.

Jina la nchi lina asili ya Kireno na linamaanisha "Mlima wa Simba".

Ni koloni la zamani la Uingereza na tangu 27 Aprili 1961 ni jamhuri huru.

Sierra Leone ni kati ya nchi maskini sana duniani.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Nchi yenyewe ilianzishwa na Waingereza kwa kuunda mji wa Freetown ("Mji wa watu huru") mwaka 1787[1]. Kusudi lake likuwa kuwarudisha Afrika watu waliowahi kuwa watumwa. Kiasili wale wakazi wa kwanza walikuwa watumwa weusi waliopewa uhuru kwa sababu walishikamana na Waingereza dhidi ya Wamarekani katika vita vya uhuru wa Marekani.

Baadaye Waingereza wapinzani wa utumwa walinunua watumwa wakiwapa uhuru na kuwapeleka Sierra Leone.

Tangu mwaka 1807 Uingereza ulikataza biashara ya watumwa (lakini utumwa wenyewe bado) na watumwa waliopatikana kwenye meli za biashara hiyo haramu walipelekwa Sierra Leone na kupewa uhuru.

Ikianzishwa na shirika la wapinzani wa utumwa Sierra Leone ikajwa koloni la kwanza la Uingereza katika Afrika ya Magharibi mwaka 1792. Kuanzia mwaka 1802 Freetown ilikuwa makao makuu ya Kiingereza kwa Afrika ya Magharibi.

Mwaka 1961 Sierra Leone ilipewa uhuru wake.

Miaka 1994 - 2002 nchi ilikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Tangu mwisho wake nchi inajengwa tena.

Wakazi asili wamegawanyika katika makabila 16, kila moja likiwa na lugha na utamaduni maalumu; kati yake makubwa zaidi ni Watemmne (35.5%) na Watembe (33.2%).

Lugha inayojulikana na asilimia 96 za wakazi ni Kikrio, aina ya Krioli ya Kiingereza iliyochanganya pia lugha mbalibali za Kiafrika. Lakini lugha rasmi ni Kiingereza.

Upande wa dini, Waislamu ni 78.5%, Wakristo ni 20.4% na wafuasi wa dini asilia za Kiafrika hawafikii 2%. Sierra Leone ni nchi isiyo na dini rasmi.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Sierra Leone | Culture, History, & People | Britannica". www.britannica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-02-26.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Taarifa za jumla
Vyombo vya habari
Trade
Tourism
Mengineyo


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sierra Leone kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.