Fransisko wa Sales
Fransisko wa Sales alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki kwa jimbo la Geneva (Uswisi). Alizaliwa Thorens-Glières (leo nchini Ufaransa) tarehe 21 Agosti 1567 akafariki Lyon tarehe 28 Desemba 1622.
Ni kati ya watu muhimu zaidi katika Urekebisho wa Kikatoliki na katika teolojia ya maisha ya kiroho.
Anaheshimiwa kama mtakatifu na mwalimu wa Kanisa. Pia kama msimamizi wa waandishi wa habari, watunzi na wanafasihi, magazeti ya Kikatoliki na mabubu-viziwi.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 24 Januari.
Yaliyomo |
[hariri] Maisha
[hariri] Utoto na ujana
Fransisko alikuwa mtoto wa kwanza wa mtawala wa Boisy, sharifu wa Savoy.
Alipata elimu bora ambayo aliikamilisha akisoma huko Paris na Padova (Italia).
Baba yake, aliyemtaka awe mwanasheria, ndiye aliyemtuma kwenye chuo kikuu cha Padova, ambako Fransisko alipata digrii, lakini pia wito wa upadri.
Kisha kurudi kwao, aliteuliwa kuwa wakili wa Seneti ya Chambéry.
[hariri] Upadri wake
Kisha kushindana na upinzani wa baba yake, alipewa upadrisho tarehe 18 Desemba 1593, akatumwa kwenye eneo la Chablais, lililotawaliwa na madhehebu ya Calvin.
Huko alijitosa hasa kuhubiria, akitumia mbinu ya majadiliano. Alipoona itikio hafifu, alibuni uandishi wa «matangazo» yaliyomwezesha kuwafikia hata watu wa mbali. Alikuwa anayabandika kutani na kuyasambaza nyumbani kwa watu kupitia chini ya milango. Hata hivyo matunda hayakuwa mengi.
Akiwa na nia ya kuzuia uenezi wa Uprotestanti kati ya Wakatoliki, aliomba kuongea na askofu wa Geneva ili kumuomba amtume akahubiri katika mji huo, makao makuu ya Wakalvini.
Kisha kufika alijadiliana na Waprotestanti ili kuwarudisha wengi iwezekanavyo kwenye umoja kamili na Kanisa la Roma.
Wazo lake kuu lilielekea daima walei wa kawaida, ili kuwapa mafundisho na miongozo ya maisha ya Kikristo.
Juhudi zake na mafanikio aliyopata kwa ubora wa mahubiri yake vilifanya ateuliwe kuwa askofu mwandamizi wa Geneva mwaka 1599, akiwa na umri wa miaka 32 tu.
[hariri] Uaskofu
Baada ya miaka mitatu akawa askofu wa jimbo hilo ambapo alijitahidi kutekeleza maagizo ya Mtaguso wa Trento.
Lakini mji ulibaki kwa jumla mikononi mwa Wakalvini, hivyo ilimpasa aishi Annecy, katika mkoa wa Savoy.
«Kama ni kukosea, napenda kukosea kwa kuzidisha wema kuliko ukali»: kauli yake hiyo inaeleza vipi aliweza kujivutia watu wengi. Ufafanuzi wake wa upendo wa Mungu ndio uliowafanya Wakalvini wengi wajiunge na Kanisa Katoliki.
Kati ya watu aliowaongoza kiroho, kuna watakatifu Vinsenti wa Paulo na Yoana Fransiska wa Chantal, aliyemsaidia kuanzisha Shirika la Maonano. Huko Thonon alianzisha pia tawi la Oratorio ya mtakatifu Filippo Neri ili kueneza utakatifu kati ya Wakristo wote.
[hariri] Maandishi
- Introduction a la vie devote par S. François de Sales eveque et prince de Geneve, Derniere edition, revue, corrigee, & augmentee, A Lyon: chez Louis Servant, 1608;
- Traicte de l'amour de Dieu par François de Sales euesque de Geneue, A Lyon, Chez Pierre Rigaud, rue Merciere, au coing de rue Ferrandiere, a l'enseigne de la fortune, 1620;
- Les epistres spirituelles du bien-heureux François de Sales euesque & prince de Geneue, ... Diuisees en sept liures. Le 1. Contenant celles qu'il a escrit aux papes, cardinaux, euesques, roys, princes. Le 2. Plusieur beaux enseignemens... Recuillies par messire Loys de Sales, preuost de l'eglise de Geneue, A Lyon, pour Vincent de Coeursilly en rue Tupin a la fleur de Lis, 1628;
- Lauro Aime Colliard, Une lettre inedite de Saint François de Sales concernant la bastonnade d'un jeune homme fort eveille, Roma, LAS, 2002, estratto da "Salesianum", a. 64. (2002), pp. 525–543.
Kati ya vitabu alivyotunga, muhimu zaidi ni "Kuingia maisha ya juhudi" na "Kitabu cha upendo wa Mungu", ambavyo ni kati ya vitabu bora vya kidini vya nyakati zote.
Kwa ajili hiyo anahesabiwa kama baba wa maisha ya kiroho ya nyakati zetu, yaliyofuatwa na watakatifu wengi, hasa Yohane Bosco, mwanzilishi wa Wasalesiani.
[hariri] Heshima baada ya kifo
Alitangazwa na Papa Alexander VII kuwa mwenye heri tarehe 8 Januari 1662, na mtakatifu tarehe 19 Aprili 1665. Halafu Papa Leo XIII mwaka 1887 alimtangaza mwalimu wa Kanisa.
[hariri] Maandishi yake katika mtandao
- Better Translation of the book, "Introduction to the Devout Life".
- Christian Classics Ethereal Library Introduction to the devout life.
- Set Your Heart Free, 30 days with a great spiritual teacher, edited by John Kirvan.
- Spiritual Conferences.
- The Catholic Controversy.
- Treatise on the Love of God.
[hariri] Viungo vya nje
- Catholic Encyclopedia: St. Francis de Sales
- International Commission on Salesian Studies All about St. Francis de Sales worldwide
- Founder Statue in St Peter's Basilica
- Francis de Sales bio at Catholic.org
|
|||||
