Antoni wa Padua
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Antoni wa Padua (Lisbon, 15 Agosti, 1195 - Padova, 13 Juni, 1231) ni mmojawapo kati ya watakatifu wanaopendwa zaidi katika Kanisa Katoliki, pia kwa sababu ya miujiza mingi inayopatikana kwa kukumbilia maombezi yake.
Kwanza alijiunga na shirika la Agostino wa Hippo huko Coimbra (1210) halafu alihamia lile la Ndugu Wadogo (1220); alisafiri sana akiishi Ureno, halafu Italia na Ufaransa.
Mwaka 1221 alikwenda Asizi kushiriki mkutano mkuu wa shirika, alipokutana na mwanzilishi, Fransisko wa Asizi.
Mtu mnyenyekevu sana, ingawa mwenye hekima na elimu kubwa, aliagizwa na Fransisko kufundisha teolojia huko Bologna. Kutokana na uwezo wake katika kuhubiri, aliagizwa pia kwenda kuzuia uenezi wa uzushi wa Wakatari huko Ufaransa.
Hatimaye alihamishiwa Padua, alipofariki akiwa na umri wa miaka 36 tu.
Alitangazwa mtakatifu na Papa Gregori IX tarehe 13 Mei 1232, na mwalimu wa Kanisa na Papa Pius XII mwaka 1946 aliyempa jina la Doctor Evangelicus (Mwalimu wa Kiinjili), kutokana na mafundisho yake kujaa roho na maneno ya Injili ya Yesu Kristo.
[hariri] Viungo vya nje
- Mahubiri yote ya Mt. Antoni yaliyotunwa hadi leo kwa Kilatini na Kiitalia
- Maandishi yote ya Mt. Antoni
|
|
|---|
| Atanasi • Efrem • Ilari • Sirili wa Yerusalemu • Basili • Gregori wa Nazianzo • Ambrosi • Jeromu • Yohane Krisostomo • Augustino • Sirili wa Aleksandria • Leo • Petro Krisologo • Gregori Mkuu • Isidori • Yohane wa Damasko • Beda • Petro Damiani •
Anselmi • Bernardo • Alberto • Antoni wa Padua • Bonaventura • Thoma wa Akwino • Katerina • Teresa wa Yesu • Petro Kanisio • Yohane wa Msalaba • Roberto Bellarmino • Laurenti wa Brindisi • Fransisko wa Sales • Alfonso Maria • Teresa wa Mtoto Yesu |