Anselm wa Canterbury
Anselm wa Canterbury (ambaye alizaliwa Aosta, leo nchini Italia, takriban 1033 au 1034 – akafariki tarehe 21 Aprili 1109) alikuwa kati ya wanafalsafa na wanateolojia muhimu wa zama za kati za Ulaya.
Baada ya kujiunga na monasteri wa Wabenedikto wa Bec huko Ufaransa alichaguliwa (1093) kuwa askofu mkuu wa Canterbury (Uingereza).
Mwaka 1163 alitangazwa kuwa mtakatifu.
Mwaka 1720 alitangazwa na Papa Klementi XI kuwa Mwalimu wa Kanisa kutokana na ubora wa maandishi yake yaliyomfanya ajulikane kama mwanzilishi wa teolojia ya shule .
Sikukuu yake ni 21 Aprili.
Yaliyomo |
[hariri] Maisha
[hariri] Utoto na ujana
Anselm alizaliwa mjini Aosta[1] au karibu nao [2] Aosta katika ufalme wa Burgundy (leo katika mkoa wa Valle d'Aosta, inapotumika lugha ya Kifaransa nchini Italia) mwaka 1033 au 1034.[1] Familia yake ilikuwa tajiri na ya kisharifu na upande wa mama ilihusiana na watawala wa Savoy[3]).
Baba yake, Gundulf de Candia, mwenye asili ya Kilombardia, alikuwa mkali, tofauti na na mama, Ermenberga wa Geneva.
Alipofikia umri wa miaka 15, Anselm alitamani kuingia monasteri, lakini hakuruhusiwa.[1] Jambo hilo lilimfanya augue; kisha kupona aliacha masomo na kuishi kistarehe tu. Wakati huo mama alifariki na baba alizidi kuwa mkali.
Alipofikia miaka 23, Anselm aliondoka nyumbani, akavuka milima ya Alps na kutangatanga katika Burgundy na Ufaransa.[2] Akivutiwa na sifa ya Lanfranc (priori wa Abasia ya Bec), Anselm alikwenda Normandy mwaka 1059. Mwaka uliofuata, kisha kuishi kidogo huko Avranches, aliingia rasmi malezi ya kitawa kama mnovisi akiwa na miaka 27; miaka iliyofuata kanuni ya Benedikto wa Nursia iliathiri kabisa mawazo na maisha yake.[4]
[hariri] Miaka huko Bec hadi Canterbury
Mwaka 1063, Lanfranc aliteuliwa abati wa Caen na Anselm priori wa Bec.[5] Anselm alishika nafasi hiyo kwa miaka 15 halafu akawa abati kutokana na kifo cha Herluin wa Bec, mwanzilishi wa abasia hiyo, kilichotokea mwaka 1078. Aliwekwa wakfu tarehe 22 Februari 1079 na askofu wa Evreux.[6]
Chini ya Anselm, Bec ikawa kituo bora cha elimu Ulaya, ikivuta wanafunzi kutoka nchi mbalimbali,[7] ingawa masomo hayakuwa na nafasi ya kwanza katika umonaki.[8]
Akiwa Bec aliandika vitabu vya kwanza vya falsafa, Monologion (1076) na Proslogion (1077–8). Hivyo vilifuatwa na Majadiliano kuhusu Ukweli, Hiari na Anguko la Ibilisi.
Wakati huo alijitahidi pia kulinda uhuru wa abasia dhidi ya mamlaka za nje.[9]
Mara kadhaa Anselm alitembelea Uingereza ili kusimamia mali za abasia na kumuona Lanfranc, hadi huyo alipofariki mwaka 1089.[10] Kwa kuwa alithaminiwa na wenyeji wa huko, mwenyewe alichaguliwa kushika nafasi ya Lanfranc kama Askofu mkuu wa Canterbury.
[hariri] Askofu mkuu wa Canterbury
Kuanzia mwaka 1093 alipopata kuwa askofu mkuu wa Canterbury, alishindana mara kadhaa na wafalme wa Uingereza Williamu II na Henri I, na kwa sababu hiyo mara mbili ilimpasa kwenda uhamishoni. Upatanisho kati ya mfalme na papa ulimwezesha kurudi Canterbury, alipofariki mwaka 1109.
Kitabu maarufu zaidi alichokiandika miaka hiyo ya mwisho kati ya Uingereza na Italia, kinaitwa Cur Deus homo (Kwa nini Mungu kuwa mtu?). Anselm aliacha pia mkusanyo mkubwa wa Sala na wa Tafakuri, mbali na Barua nyingi, ambazo zinawezesha kuona pia mafungamano ya kirafiki aliyokuwa nayo kwa wanafunzi wake.
Anselm anakumbukwa si tu kama mwanateolojia, bali pia kama mwanafalsafa, hasa kwa utafiti wake katika Proslogion, kuhusu unum argumentum, yaani hoja kuu inayojitegemea na kujitosheleza katika kuthibitisha uwepo wa Mungu na sifa zake.
[hariri] Imani na akili
Mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuchimba nadharia, Anselm alitafuta, kwa kufuata nyayo za Plato na Agostino wa Hippo, namna ya kukutanisha imani na akili. Kwake, akili ya binadamu ni chombo muhimu cha utafiti wa teolojia. Bila ya shaka, anadai kwanza imani, akisema "nasadiki ili nielewe, na nisiposadiki kwanza sitaweza kuelewa. Hivyo, Anselm alirithi kwa Agostino kauli credo ut intelligam, intelligo ut credam (yaani "nasadiki ili nielewe, naelewa ili nisadiki"). Utafiti wa ukweli unategemea imani, lakini hiyo peke yake haitoshi, bali inadai pia aina mbalimbali za uthibitisho wa akili. Katika hilo akili, sawa na imani yenyewe, ana mwongozo wa hakika katika mwanga wa Mungu ambao usipokuwepo akili haiwezi kabisa kupenya fumbo la Mungu. Kwa maneno mengine, akili haitoi matamko, bali inasaidia kuelewa imani. Anselm ni kati ya wataalamu wa kwanza waliounganisha falsafa na teolojia, kadiri ya neno fides quaerens intellectum (yaani "imani inadai akili"), litakalokuwa msingi wa teolojia ya shule.
[hariri] References
- ↑ 1.0 1.1 1.2 Walsh, Michael, ed. Butler's Lives of the Saints. (HarperCollins Publishers: New York, 1991), pp. 117
- ↑ 2.0 2.1 Charlesworth, M. J., trans. and ed. St. Anselm's Proslogion. (University of Notre Dame Press: Notre Dame, 2003), pp. 9.
- ↑ R. Southern. St. Anselm: Portrait in a Landscape. (Cambridge University Press: 1992), pp. 8. http://books.google.com/books?hl=en&lr=&id=lxf-LvQvvwIC&oi=fnd&pg=PR15&dq=anselm+of+canterbury+r-southern&ots=e6-_fZ6v0B&sig=3rOwM0tvC4VVInlSWl099J0dyjE#PPA8,M1
- ↑ R. Southern. St. Anselm: Portrait in a Landscape. (Cambride University Press: 1992), pp. 32. http://books.google.com/books?hl=en&lr=&id=lxf-LvQvvwIC&oi=fnd&pg=PR15&dq=anselm+of+canterbury+r-southern&ots=e6-_fZ6v0B&sig=3rOwM0tvC4VVInlSWl099J0dyjE#PPA8,M1
- ↑ Charlesworth, M. J., trans. and ed. St. Anselm's Proslogion. (University of Notre Dame Press: Notre Dame, 2003), pp. 10.
- ↑ Vaughn, Sally. "St Anselm of Canterbury: the philosopher-saint as politician." Journal of Medieval History. 1 (1975), 279–306: 282.
- ↑ Charlesworth, M. J., trans. and ed. St. Anselm's Proslogion. (University of Notre Dame Press: Notre Dame, 2003), pp. 15.
- ↑ Charlesworth, M. J., trans. and ed. St. Anselm's Proslogion. (University of Notre Dame Press: Notre Dame, 2003), pp. 13.
- ↑ Vaughn, Sally. "St Anselm of Canterbury: the philosopher-saint as politician." Journal of Medieval History. 1 (1975), 279–306: 281.
- ↑ Charlesworth, M. J., trans. and ed. St. Anselm's Proslogion. (University of Notre Dame Press: Notre Dame, 2003), pp. 16.
[hariri] Viungo vya nje
- "St. Anselm of Canterbury (1033—1109)" article by Greg Sadler in the Internet Encyclopedia of Philosophy
- Professor Jasper Hopkins: Anselm of Canterbury containing English translations of nearly every major work by St. Anselm
- "Introducing...Anselm of Canterbury". Three lectures giving an overview of Anselm's works (with particular reference to faith and reason) by Dr. Michael Reeves on www.theologynetwork.org
|
|||||
| Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Anselm wa Canterbury kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
