Mahututi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mahututi ni kivumishi cha sifa chenye asili ya Kiarabu ambacho huambatana sana na nomino mgonjwa.

Tunaposema mgonjwa mahututi basi tunamaanisha ni mtu aliye katika hali mbaya kwa sababu ya ugonjwa. Huenda yule mtu akawa katika kitengo cha hospitali kwa ajili ya huduma za pekee (sadaruki; kwa Kiingereza: Intensive Care Unit, kipufi: ICU) au akawa nyumbani akitazamiwa kufa.

Mwambatanisho wa maneno haya hutumika pia baada ya ajali ambapo, waliojeruhiwa sana na huenda wakaaga dunia kwa majeraha na mshtuko baada ya ajali husemwa kuwa mahututi.

Hali hiyo inadai mtu atendewe kwa utaalamu na wema wa pekee.

Dini mbalimbali zinaelekeza namna ya kumhudumia hata kiroho, kwa mfano Wakristo wa madhehebu mbalimbali wanampatia kitubio, mpako wa wagonjwa na komunyopamba.

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mahututi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.