Hilari wa Poitiers

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Hilari akiwekwa wakfu kuwa Askofu wa Poitiers.

Hilari wa Poitiers (315 hivi - 367), askofu wa Pictavium (leo Poitiers), mwanateolojia, mwanafalsafa na mwandishi, anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu na babu wa Kanisa.

Wakatoliki wanamheshimu pia kama mwalimu wa Kanisa tangu mwaka 1851.

Sikukuu yake inaadhimisha tarehe 13 Januari.

[hariri] Maisha

Akizaliwa katika familia ya kisharifu, Hilari alivutiwa mapema na falsafa.

Alikuwa baba wa nyumbani alipochaguliwa askofu wa Poitiers mwaka 353.

Mwaka 354 tu alikuja kujua Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli, akaanza kuitetea katika sinodi na mitaguso dhidi ya uzushi wa Waario.

Kwa ajili hiyo mwaka 356 alipelekwa na kaisari Kostanzo II uhamishoni Frigia (leo katika Uturuki).

Huko miaka mitano iliyofuata alipata nafasi ya kuchimba mafundisho ya mababu wa Kanisa wa mashariki, hata akaweza kuandika juu ya Utatu (De Trinitate).

[hariri] Maandishi

  • De Trinitate ndio kitabu chake bora; kilikuwa cha pekee katika Kilatini
  • Tenzi
  • Contra Arianos vel Auxentium Mediolanensem liber
  • Contra Constantium Augustum liber
  • Commentarius in Evangelium Matthaei
  • Tractatus super Psalmos

[hariri] Viungo vya nje

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hilari wa Poitiers kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine