Petro Krisologo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Petro Krisologo katika mavazi ya askofu mkuu.

Petro Crisologo (Imola, Italia, 406 - Imola, 2 Desemba 450) alikuwa askofu mkuu wa Ravenna (mkoa wa Emilia-Romagna huko Italia kaskazini).

Tangu zamani anaheshimiwa kama mtakatifu na babu wa Kanisa.

Mwaka 1729 Papa Benedikto XIII alimuongezea sifa ya mwalimu wa Kanisa.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 30 Julai.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alipewa ubatizo, malezi na daraja takatifu ya ushemasi na Korneli, askofu wa Imola.

Papa Sixtus III alimteua kuwa askofu wa Ravenna mwaka 433. Chini yake Kanisa la mji huo likawa jimbo kuu.

Ni kati ya wachungaji bora wa wakati ule, akitekeleza mwenyewe kipeo cha askofu alichokichora hivi: “Kuwa ndani ya Kristo mtumishi huru wa wote”

Uadilifu na ari yake vilimvutia waamini wengi waliomuita Krisologo (kutoka Kigiriki, "Neno la dhahabu") kwa sababu ya mvuto wa kiroho na ufasaha wa mahubiri yake.

Maandishi[hariri | hariri chanzo]

Tuna hotuba 183 za Petro, hasa za kufafanulia Biblia na za kumsifu Bikira Maria na Yohane Mbatizaji.

Petro alifafanua vizuri hasa fumbo la Umwilisho na Kanuni ya Imani ya Mitume, akipinga uzushi wa Ario na ule wa Eutike. Alimuandikia huyo ili akubali maamuzi ya Papa Leo I.

Maandishi yake[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]