Mtakatifu Ireneo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mt. Irenaeus, Askofu wa Lyon.

Mtakatifu Ireneo (130200) alikuwa askofu wa mji wa Lyon nchini Ufaransa.

Ametambuliwa kuwa mtakatifu kama mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 28 Juni.

Maisha [hariri]

Ireneo alizaliwa yapata mwaka 130.

Alilelewa katika mji wa Smirna (leo İzmir nchini Uturuki), akiwa ni mwanafunzi wa Mt. Polikarpo aliyekuwa askofu wa mji huo.

Mwaka 177, baada ya kuhamia Ufaransa, Ireneo alipata upadri huko Lyons, na baadaye kidogo aliteuliwa kuwa askofu wa hapo.

Ni muhimu kwa juhudi zake za kupigania umoja wa Kanisa.

Katika maandishi yake alijitahidi sana kutetea imani ya kikatoliki dhidi ya mafundisho ya Wagnostiki.

Kwa mujibu wa mapokeo, aliifia dini yake mnamo mwaka 200.

Marejeo [hariri]

  • (1885) The Ante-Nicene Fathers. Buffalo, NY: The Christian Literature Company. 
  • Eusebius (1932). The Ecclesiastical History, Kirsopp Lake and John E.L. Oulton, trans, New York: Putnam. 
  • Hägglund, Bengt (1968). History of Theology, Gene J.Lund, trans, St. Louis: Concordia Publishing. 
  • Minns, Denis (1994). Irenaeus. Washington, D.C.: Georgetown University Press. ISBN 0878405534. 
  • Payton Jr., James R. Irenaeus on the Christian Faith: A Condensation of 'Against Heresies' (Cambridge, James Clarke and Co Ltd, 2012).
  • Quasten, J. (1960). Patrology: The Beginnings of Patristic Literature. Westminster, MD: Newman Press. 
  • Schaff, Philip (1980). History of the Christian Church: Ante-Nicene Christianity, A.D. 100-325. Grand Rapids, Mich: Eerdmans. ISBN 0802880479. 
  • Tyson, Joseph B. (1973). A Study of Early Christianity. New York: Macmillan. 
  • Wolfson, Henry Austryn (1970). The Philosophy of the Church Fathers: Faith, Trinity, Incarnation. Cambridge, MA: Harvard University Press. 

Viungo vya nje [hariri]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtakatifu Ireneo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.