Mtume Yohane

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Yohane mtume na mwinjili (mchoro wa Simone Martini)

Yohane mwana wa Zebedayo alikuwa mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu, ambaye alipendwa na mwalimu wao kuliko wote.

Mapokeo ya Kikristo yanamuona kuwa mwandishi wa Injili ya Yohane, wa barua tatu (Waraka wa kwanza wa Yohane, Waraka wa pili wa Yohane, Waraka wa tatu wa Yohane) na wa Kitabu cha Ufunuo.

Mitume wa Yesu

Alizaliwa na Salome baada ya mtume Yakobo Mkubwa mwanzoni mwa karne ya 1 B.K. akafa mkongwe mwishoni mwa karne hiyo huko Efeso.

Kabla ya kumfuata Yesu Kristo alikuwa mfuasi wa Yohane Mbatizaji.

Ndiye shahidi mkuu wa miaka mitatu hivi ya utume wa Yesu, akiwa wa kwanza kumfuata (pamoja na Mtume Andrea), mshiriki wa matukio ya pekee ya mwalimu wake (kama alipogeuka sura mlimani), mtume pekee aliyesimama chini ya msalaba, wa kwanza kusadiki ufufuko wa Yesu hata kabla hajamuona.

Kutokana na udhati wa teolojia yake alifananishwa na tai.

[hariri] Viungo vya nje

http://www.newadvent.org/cathen/08492a.htm katika Catholic Encyclopedia (1913)