Yakobo Mkubwa
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yakobo, mwana wa Zebedayo na Salome, na kaka wa Mtume Yohane, alikuwa mmoja kati ya Mitume wa Yesu muhimu zaidi.
Anaitwa "Mkubwa" ili kumtofautisha na Mtume mwingine mwenye jina hilohilo, Yakobo Mdogo mwana wa Alfayo.
Yaliyomo |
[hariri] Maisha ya awali
Yakobo pamoja na baba na mdogo wake walikuwa wavuvi huko Kafarnaumu kwenye Ziwa la Galilaya.
Wataalamu kadhaa wanadhani walikuwa pia makuhani.
| Mitume wa Yesu |
|---|
|
[hariri] Wito wa utume
Inakadiriwa alikutana na Yesu mwaka 28.
Pamoja na mdogo wake waliitwa na Yesu Boanerghes ("wanangurumo") kutokana na umotomoto wao.
Pamoja na mitume wengine waliongozana na Yesu Kristo miaka mitatu hivi, ambapo Yakobo alionekana kuwa karibu sana na Yesu na kuchaguliwa naye kushuhudia matukio kadhaa ya pekee (ufufuo wa binti Yairo, kugeuka sura mlimani, kihoro bustanini).
[hariri] Baada ya ufufuko wa Yesu
Baada ya kifo na ufufuko wa Yesu, Yakobo alishika nafasi ya maana katika jumuia ya kwanza ya Wakristo wa Yerusalemu.
Mwaka 43 hivi aliuawa na Herode Agripa I kwa upanga (Matendo ya Mitume 12:1-2), wa kwanza kumfia Yesu kati ya Mitume wake.
[hariri] Heshima yake
Anaheshimiwa na Wakristo wote kama mtakatifu, hasa tarehe 25 Julai huko Santiago de Compostella (Hispania, ambapo wengi wanaamini aliwahi kufika kiutume).