Mtume Bartolomayo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mitume wa Yesu

Bartolomayo (kwa Kigiriki Βαρθολομαιο&sigma) ni jina la mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu kadiri ya Injili Ndugu.

Wengi wanaona hilo ni ubini wake (kwa Kiaramu lina maana ya "mwana wa Tolomayo"), kumbe jina lake mwenyewe ni "Natanaeli", kama anavyotajwa na Injili ya Yohane 1:45 rafiki wa Mtume Filipo. Kama ni hivi, alikuwa mwenyeji wa Kana ya Galilaya, na unyofu wake ulisifiwa na Yesu.

Yote tunayoyajua kwa hakika juu yake yanategemea Injili na Matendo ya Mitume anapotajwa tu katika orodha ya Thenashara ambao waliteuliwa na Yesu Kristo kama mwanzo mpya wa taifa la Mungu wakatumwa naye kuhubiri na kuponya.

Baada ya ufufuko wa Yesu na Pentekoste, hakuna habari za hakika, ila kuna masimulizi ya utume wake Mashariki ya Kati hadi India.

Alifia dini ya Ukristo katika nusu ya pili ya karne I labda Syria au Armenia. Anaheshimiwa hasa tarehe 24 Agosti.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Thenashara, Mitume Kumi na Wawili – tafsiri ya P. A. Bunju – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Ndanda 1984 – ISBN 9976-63-030-1
  • Easton's Bible Dictionary, 1897.
  • Encyclopedia Anglicana, 1911
  • Dictionary of First Names, Patrick Hanks and Flavia Hodges. Oxford University Press, 1996
  • Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-14-051312-4.
  • The Apostles In India by Fr A.C Perumalil SJ 1952
  • For a discussion of Baroque paintings of St. Bartholomew by the Spanish artist Ribera, see: Williamson, Mark A. "The Martyrdom Paintings of Jusepe de Ribera: Catharsis and Transformation", PhD Dissertation, Binghamton University, Binghamton, New York 2000 (available online at myspace.com/markwilliamson13732)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: