Mtume Thoma
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Mitume wa Yesu |
|---|
|
Thoma au Didimo, yaani Pacha ni jina la mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu anayeheshimiwa kama mtakatifu, kwa namna ya pekee na Wakristo wa maeneo yaliyokuwa mashariki kwa Dola la Roma, kuanzia Iraq hadi India.
Inawezekana sababu yake ni kazi alizofanya huko hadi kifodini chake huko Chennai (Tamil Nadu) mwaka 72.
Alikuwa mtu mwenye tabia ya pekee iliyomvutia umaarufu hadi leo. Hasa alielekea kukata tamaa, kupinga hoja na kutosadiki kwa urahisi.