Mtume Andrea

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kifodini cha Mtume Andrea msalabani

Mtume Andrea alikuwa mmoja kati ya Mitume wa Yesu.

Anaheshimiwa na Wakristo wote hasa tarehe 30 Novemba. Ni msimamizi wa Scotland, Russia, Ugiriki, Romania, Malta, Prussia, na wa mabaharia, wavuvi, na waimbaji.

Mitume wa Yesu

Yaliyomo

Asili na jina [hariri]

Inakadiriwa alizaliwa mwaka 6 K.K. huko Betsaida akauawa 60 (hivi) huko Patrasso (Ugiriki).

Jina lake asili la Kiyahudi halijulikani. Kwa Kigiriki aliitwa Ανδρέας (Andreas, maana yake Mwanamume, Rijali). Anaitwa pia Protocletos yaani Wa kwanza kuitwa (na Yesu).

Agano Jipya linasema Andrea alikuwa ndugu wa Mtume Petro, mwana wa Yona au Yohana (Mathayo 16:17; Yohane 1:42).

Wito wake [hariri]

Wote wawili walihamia Kafarnaumu ili kufanya kazi ya uvuvi, na ndipo walipoitwa kuwa "wavuvi wa watu" (ἁλιείς ἀνθρώπων, halieis anthropon).

Injili ya Yohane inaarifu kuwa Andrea aliwahi kuwa mwanafunzi wa Yohane Mbatizaji, mpaka nabii huyo alipomuelekeza amfuate Yesu Kristo, "Mwanakondoo wa Mungu" atakayekamilisha kazi yake (Yohane 1:35-40). Andrea akiwa wa kwanza kumtambua Yesu kuwa Masiya, alimtambulisha kwa ndugu yake (Yohane 1:41).

Ni baada ya hapo kwamba waliitwa kuacha yote wamfuate Yesu (Marko 1:17-18; Mathayo 4:19-20; Luka 5:11).

Baada ya ufufuko wa Yesu [hariri]

Katika Injili Andrea anatajwa mara kadhaa kuwa karibu sana na Yesu (Marko 13:3; Yohane 6:8, 12:22), lakini katika Matendo ya Mitume anatajwa mara moja tu, katika orodha ya Mitume (1:13).

Eusebius wa Kaisarea anataja Asia Ndogo, Scizia, pwani ya Bahari Nyeusi na mto Volga hadi Kiev kuwa mahali pa utume wake baada ya ufufuko wa Yesu.

Mapokeo yanadai alisulubiwa huko Patrasso juu ya msalaba wenye umbo la X uliopewa jina lake.

Apokrifa za Andrea [hariri]

Kati ya vitabu vilivyokataliwa na Kanisa (Decretum Gelasianum ya Papa Gelasio I) kuna Injili ya Andrea na Matendo ya Andrea ya karne ya 3.

Picha [hariri]

Marejeo [hariri]

Viungo vya nje [hariri]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: