Mtume Filipo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kifodini cha Mt. Filippo, 1639, José de Ribera.

Filipo (kwa Kigiriki Φίλιππος, Philippos) ni jina la mfuasi wa Yesu Kristo anayeshika nafasi ya tano katika orodha zote nne za Mitume wa Yesu katika Agano Jipya.

Habari zake zinapatikana hasa katika Injili na Matendo ya Mitume.

Mitume wa Yesu

Ndiye aliyemleta kwa Yesu rafiki yake Natanaeli (Injili ya Yohane 1:43-46).

Baadaye aliulizwa na Kristo bei ya mikate inayohitajiwa na umati kabla hajawazidishia ile michache iliyokuwepo (Yoh. 6:5-7}.

Pia alimletea Yesu Wagiriki ambao walifika Yerusalemu kwa ajili ya Pasaka wakataka kumfahamu (Yoh. 12:20-22).

Hatimaye, katika karamu ya mwisho ya Yesu na mitume wake alimuomba awaonyeshe Baba (Yoh. 14:8) akalaumiwa naye kwa kutomtambua ndani yake (Yoh. 14:9).

Eusebio wa Kaisarea, katika Historia ecclesiastica, iii.39, aliripoti maneno ya Papia, askofu wa Hierapolis kwamba Filipo alikuwa na mke na watoto na kwamba alifia Hierapolis (mwaka 80 hivi).

Anaheshimiwa kama mtakatifu na Kanisa Katoliki na madhehebu mengine yote ya Ukristo yanayokubali heshima hiyo, lakini kwa tarehe tofauti.

[hariri] Viungo vya nje

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine