Papias
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Papias wa Hierapoli (* mnamo 70; † mnamo 140) alikuwa askofu au kiongozi wa ushirika wa kikristo mjini Hierapoli (karibu na Pamukkale ya leo katika Uturuki).
Papias ni maarufu katika historia ya Ukristo wka sababu yeye ni mtu wa kanza anayejulikana alikusanya habari juu ya waandishi wa Agano Jipya. Aliandika habari hizi katika vitabu vitano vilivyoitwa "Maelezo kuhusu maneno ya Bwana (Yesu)". Maandiko haya yamepotea lakini sehemu ya yaliyomo yake zimehifadhiwa katika vitabu vingine vya Irenaeo (Dhidi uzushi) na Eusebio wa Kaisaria walikuwa na vitabu vyake wakati wa kuandiki miandiko yao.
Umuhimu wa Papias ni yeye alikuwa mwandishi wa kale anayejulikana baada ya waandishi wa Biblia wenyewe aliyeshika habari zao.
Papias alimtaja Mtume Mathayo kama mwandishi wa Injili ya Mathayo na "Presbiteri Marko mfasiri wa Petro" kama mwandishi wa Injili ya Marko.
Waandishi wa baadaye katika Ukristo wa kale hawakukubaliana juu yake. Wengine walimsifu wengine waliwona kama mtu asiye na habari za maana.
[hariri] Viungo vya Nje
- Hieropolis/Pamukkale
- Paul N. Tobin, "The Apostolic Succession: Polycarp and Clement": A skeptical assessment finds inconsistencies in Irenaeus' interpretation of Papias' apostolic connection, as reported in this article.