Upanga
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Upanga wa mikono miwili kwenye makumbusho ya Dresden
Upanga ni silaha inayoshikwa mkononi. Hutengenezwa kwa metali hasa feleji ikifanana na kisu ila tu ni kubwa. Hasa kengee yake ni ndefu na mpini wake ni mkubwa kwa sababu mkono wote unahitaji kushika silaha hii.
Mara nyingi kuna chuma cha kupandana kinachokusidiwa kukinga mkono unaoshika upanda. Umbo la upanga ni muhimu kwa mbinu za mapigano.
Kuna aina nyingi za upanga zinazotofautiana hasa katika urefu na pia uzito.
Panga za kwanza zilitengenezwa na wahunzi wa Misri na China wakitumia bronzi. Tangu kupatikana kwa bunduki umuhimu wa upanga umepungua. Katika vita ya silaha za kisasa panga zimepotea kabisa. Lakini katika vita za wenyewe kwa wenyewe kama Rwanda au ghasia ya Kenya ya 2008 panga zilikuwa silaha muhimu tena.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
| Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Upanga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |