Mwalimu wa Kanisa
Mwalimu wa Kanisa ni jina la heshima ambalo kwa nadra Kanisa Katoliki linampa mtakatifu ambaye katika maisha, mafundisho na maandishi yake alionyesha na kueneza mwanga wa pekee katika masuala ya imani, maadili na maisha ya kiroho.
Utaratibu [hariri]
Jina hilo linatolewa na Papa au Mtaguso. Mpaka sasa, katika miaka karibu 2000 ya historia ya Kanisa wanaume 31 na wanawake 4 tu wamepewa heshima hiyo.
Wa kwanza kutangazwa (mwaka 1298) ni mababu wa Kanisa wanne muhimu zaidi upande wa Magharibi: Ambrosi wa Milano, Agostino wa Hippo, Jeromu na papa Gregori I.
Mwaka 1568 walitangazwa mababu wa Kanisa wanne muhimu zaidi upande wa Mashariki: Atanasi wa Aleksandria, Basili Mkuu, Gregori wa Nazienzi na Yohane Krisostomo, pamoja na Thoma wa Akwino, mwalimu bora wa Karne za Kati upande wa Magharibi.
Halafu mapapa wakaendelea kuongeza wengine.
Orodha [hariri]
Mwaka wa kutangazwa ukifuatwa na nyota unaonyesha watakatifu wanaoheshimiwa na Waorthodoksi pia, ingawa kwao hakuna cheo cha mwalimu wa Kanisa.
- Papa Gregori I, (540 - 604) - 1298 *
- Ambrosi wa Milano (340 hivi - 397) - 1298 *
- Agostino wa Hippo, Doctor Gratiae (354 - 430) - 1298 *
- Jeromu (347 - 420) - 1298 *
- Yohane Krisostomo (350 hivi - 407) - 1568 *
- Basili Mkuu (329 hivi- 379) - 1568 *
- Gregori wa Nazianzo (329 - 390) - 1568 *
- Atanasi wa Aleksandria (295 - 373) - 1568 *
- Thoma wa Akwino, Doctor Angelicus (1225 - 1274) - 1568
- Bonaventura wa Bagnoregio, Doctor Seraphicus (1220 hivi - 1274) - 1588
- Anselm wa Canterbury, Doctor Magnificus (1033 hivi - 1109) - 1720
- Isidori wa Sevilia (560 - 636) - 1722 *
- Petro Krisologo (406 - 450) - 1729 *
- Papa Leo I, (400 hivi - 461) - 1754 *
- Petro Damiani (1007 - 1072) - 1828
- Bernardo wa Clairvaux, Doctor Mellifluus - (1090 - 1153) - 1830
- Ilari wa Poitiers (315 hivi - 367) - 1851 *
- Alfonso Maria wa Liguori, Doctor Zelantissimus (1696 - 1787) - 1871
- Fransisko wa Sales, Doctor Caritatis - (1567 - 1622) - 1877
- Sirili wa Aleksandria, Doctor Incarnationis (376 - 444) - 1883 *
- Sirili wa Yerusalemu (315 - 386) - 1883 *
- Yohane wa Damasko (650 hivi - 749) - 1883 *
- Beda Mheshimiwa - (672 - 735) - 1899 *
- Efrem Mshamu (306 - 373) - 1920 *
- Petro Kanisio (1521 - 1597) - 1925
- Yohane wa Msalaba, Doctor Mysticus (1542 - 1591) - 1926
- Roberto Bellarmino (1542 - 1621) - 1931
- Alberto Mkuu, Doctor Universalis (1193 hivi - 1280) - 1931
- Antoni wa Padua, Doctor Evangelicus (1195 - 1231) - 1946
- Laurenti wa Brindisi, Doctor Apostolicus (1559 – 1619) - 1959
- Teresa wa Yesu (1515 - 1582) - 1970
- Katerina wa Siena (1347 - 1380) - 1970
- Teresa wa Mtoto Yesu, Doctrix Amoris (1873 - 1897) - 1997
- Yohane wa Avila, (1500 - 1569) - 2012
- Hildegarda wa Bingen, (1098 - 1179) - 2012