Nenda kwa yaliyomo

Polikarpo Mtakatifu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Polikarp Mtakatifu)
Polikarp Mtakatifu

Mtakatifu Polikarpo (takriban 69-155) alikuwa askofu katika mkoa wa Asia (Uturuki wa leo).

Tangu kale anatambuliwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kuwa mtakatifu kama mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 23 Februari[1].

Polikarpo alikuwa mwanafunzi wa mtume Yohane na askofu wa mji wa Smirna (leo Izmir nchini Uturuki). Pengine barua kwa malaika wa Kanisa la Smirna inayopatikana katika Kitabu cha Ufunuo ilimlenga na kumsifu yeye.

Alikuwa rafiki wa Ignasi wa Antiokia ambaye alimuandikia barua maarufu.

Alikwenda Roma, Italia, kuzungumza na Papa Anicetus kuhusu maadhimisho ya Pasaka ili kudumisha umoja wa Kanisa katika tofauti za desturi.

Mwaka 155, chini ya makaisari Marko Antonino na Komodo, aliifia dini yake kwa kuchomwa moto katika uwanja wa michezo mbele ya gavana na umati wa watu. Habari za kifodini hicho zinasifiwa kwa uzuri wake.

Sala yake wakati wa kufia dini

[hariri | hariri chanzo]

Ee Bwana, Mwenyezi Mungu, Baba wa Mwanao mpenzi na mbarikiwa Yesu Kristo, ambaye kwa njia yake tumekufahamu; Mungu wa malaika na wa wenye uwezo, wa kila kiumbe na wa kizazi chote cha waadilifu wanaoishi mbele yako: mimi nakubariki kwa kuwa siku hii na saa hii umenijalia nishiriki kikombe cha Kristo wako pamoja na wafiadini wote, kwa ufufuo wa roho na wa mwili katika uzima wa milele, katika hali ya kutoharibika kwa njia ya Roho Mtakatifu.

Niweze leo kupokewa pamoja nao mbele yako kama sadaka nono na ya kupendeza, kama vile wewe, Mungu usiye na hila na msemakweli, ulivyoiandaa ukanionyesha mapema na sasa umeitimiza.

Kwa sababu hiyo na kwa mambo yote mimi nakusifu, nakuhimidi, nakutukuza pamoja na kuhani wa milele na wa kimbingu Yesu Kristo, Mwanao mpenzi, ambaye kwa njia yake kwako na kwa Roho Mtakatifu uwe utukufu sasa na nyakati zijazo. Amina.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1295
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.