Gavana
Gavana (Kiing. governor - mwenye kutawala) ni cheo cha kiongozi wa kisiasa au kiutawala kwenye ngazi mbalimbali.
Yaliyomo |
[hariri] Gavana kama waziri mkuu wa jimbo katika shirikisho
Kuna nchi ambako gavana ni mtendaji mkuu wa serikali katika dola la shirikisho au jimbo. Kwa mfano katika Marekani ina madola 50 ndani yake na kila moja huwa na gavana kama mkuu wa serikali ya kidola. Cheo hiki kinalingana na waziri mkuu wa sehemu ya nchi yenye kiwango cha kujitawala na bunge lake pamoja na serikali ya kieneo kwa mfano waziri mkuu wa jimbo la Afrika Kusini au Ujerumani.
[hariri] Gavana kama mtendaji mkuu wa mkoa
Katika nchi kama Japani au Indonesia watendaji wakuu wana cheo cha gavana wakichaguliwa na wanachi na kuwajibika kwa wananchi hata kama madaraka ya mikoa yao hayalingani na jimbo au dola la shirikisho.
Katika nchi nyingine magavana ni maafisa wa serikali kuu wanaoteuliwa na rais wa taifa au waziri wake kuwa watendaji wakuu katika mkoa. Hawawajibiki kwa wananchi wa eneo lao lakini kwa serikali kuu. Mfano ni gavana katika Urusi. Nafasi hii inalingana na mkuu wa mkoa katika Kenya au Tanzania tangu uhuru.
[hariri] Gavana ya koloni na katika Jumuiya ya Madola
Gavana ilikuwa cheo cha kihistoria kutoka zamani ya ukoloni kwa mkuu wa koloni anayewakilisha na serikali kuu na kuwa mkuu wa serikali katika koloni.
Cheo hikikimebaki katika Jumuiya ya Madola nchi nyingi zinamkubali malkia wa Uingereza kama mkuu wa dola na yeye anawakilishwa katika nchi hizi na afisa mwenye cheo cha "gavana mkuu".
[hariri] Gavana katika kampuni ya umma na taasisi
Katika nchi zinazotumia Kiingereza kunapia maafisa wanaoitwa gavana nje ya siasa.
- mtendaji mkuu wa benki kuu mara nyingi huitwa gavana
- katika Uingereza wasimamaizi wa magereza huitwa "prison governor"
- wasimamizi wa kimkoa wa shule wakati mwingine wanaitwa "school governor"
- taasisi mbalimbali wanasimamiwa mara nyingi na "board of governors"
| Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |