Mwanatheolojia
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwanatheolojia ni mtu anayeshughulikia theolojia au ujuzi juu ya habari za Mungu kitaalamu. Ni tofauti na mtaalamu wa dini anayeweza kuchungulia dini yoyote kwa sababu ana msimamo katika mapokeo ya dini moja hasa.
Si lazima yeye kuwa mwalimu wa dini yake anayatambuliwa na waumini kwa sababu kitambulisho ni kiwango chake cha elimu si ya imani. Hata hivyo kuna pia wanatheolojia ambao mara nyingi ni viongozi wa kiroho.
Katika mapokeo ya Ukristo wa magharibi mwanatheolojia amepita ngazi za chuo kikuu na masomo yake katika idara ya theolojia. Nje ya Ukristo wa magharibi kwa mfano katika Uislamu, Uyahudi na Ukristo wa mashariki kuna pia njia mbalimbali za kukubaliwa kufika kwenye kiwango cha utaalamu wa habari za Mungu.
Katika muundo wa theolojia ya magharibi mwanatheolojia ataweka mkazo wako katika masomo ya theolojia kama vile
- Agano la Kale
- Agano Jipya
- Historia ya Kanisa
- Mafundisho ya Imani ya Kikristo
- Mafundisho ya Maadili ya Kikristo
- Mafundisho ya habari ya kichungaji kama vile
- mahubiri ya imani
- kufundisha imani
- kuchunga roho za waumini na kaushauriana nao
na mengineyo.

