Potinus wa Lyon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kanisa la Mt. Potinus huko Lyon.

Potinus (kwa Kifaransa Saint Pothin) alikuwa askofu wa Lyon aliyeuawa mwaka 177 wakati wa dhuluma ya kaisari Marcus Aurelius dhidi ya Ukristo.

Askofu Ireneo wa Lyon alimtaja kama mtangulizi wake katika barua ambaye anadhaniwa kuwa aliwaandikia Wakristo wa mkoa wake wa asili, Asia ndogo. Kadiri yake, Potinus alizaliwa mwaka 87 huko Frigia (katika Uturuki wa leo) akatumwa na Polikarpo wa Smirna kufanya umisionari Ulaya magharibi pamoja na Wakristo wengine.

Anahesabiwa kuwa askofu wa kwanza wa Ufaransa.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]