Sirili wa Yerusalemu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mtakatifu Sirili wa Yerusalemu (315386) alikuwa askofu wa Yerusalemu.

Ametambuliwa kuwa mtakatifu na mwalimu wa Kanisa.

Sikukuu yake ni tarehe 18 Machi.

[hariri] Maisha

Sirili alizaliwa katika familia ya Kikristo mwaka 315.

Aliteuliwa kuwa Askofu wa Yerusalemu nchini Israeli mwaka 348.

Alihusika hasa na mabishano na Ario juu ya umungu wa Yesu, na kwa sababu hiyo zaidi ya mara moja alifukuzwa nchini mwake.

Moyo wake wa kichungaji unaonekana hasa katika kitabu chake Catecheses, ambamo anawaeleza watu mafundisho ya kweli ya Ukristo, Maandiko Matakatifu, na mapokeo ya Kanisa.

Alikufa mwaka 386.

[hariri] Tazama pia

[hariri] Marejeo

  • "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1300
Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sirili wa Yerusalemu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.