Canterbury
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Jiji la Canterbury | |
| Mahali pa mji wa Canterbury katika Uingereza | |
| Coordinates: 51°16′30″N 1°5′13″E / Expression error: Unexpected < operator Expression error: Unexpected < operator | |
| Nchi | Uingereza |
|---|---|
| Mkoa | South East |
| Wilaya | Kent |
| Idadi ya wakazi | |
| - Mji | 43,432 |
| Website: www.canterbury.co.uk | |
Canterbury ni mji wa mkoa wa Kent, kusini mwa Uingereza, si mbali na London. Una wakazi 42.259 (2001).
[hariri] Historia
Ulianza kukaliwa karne nyingi K.K. na kuitwa Cantuaria. Baada ya kuvamiwa na Warumi chini ya Julius Kaisari mwaka 55 K.K. ulifanywa Forum commerciale (yaani mahali pa biashara).
Kuanzia mwaka 560 ukawa mji mkuu wa ufalme wa Kijerumani wa Kent, na mwaka 597 Augustino wa Canterbury akitokea Roma akaanzisha huko dayosisi ya kwanza ya Kilatini katika kisiwa cha Britania. Kwa ubatizo wa mfalme, uinjilishaji ulipiga hatua kubwa.
Tangu hapo, mji huo ukawa na umuhimu hasa upande wa Ukristo, kwa sababu dayosisi hiyo ilizaa taratibu nyingine zote za kisiwa hicho.
Kwa msingi huo, Askofu mkuu wa Canterbury akawa mkuu wa Maaskofu wote wa Uingereza, halafu wa Waanglikana wote duniani.
[hariri] Picha
|
Askofu Thomas Becket aliuawa katika Kanisa kuu la Canterbury |