Tanganyika (ziwa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Ziwa la Tanganyika
Ziwa Tanganyika jinsi inavyoonekana kutoka angani
Ziwa Tanganyika jinsi inavyoonekana kutoka angani
Mahali Afrika ya Mashariki
Nchi zinazopakana Burundi, Kongo,
Tanzania, Zambia
Eneo la maji 32,893 km² kutegemeana na kiasi cha mvua
Kina ya chini kuanzia 3.5 m
Mito inayoingia Lufubu, Malagarasi, Ruzizi
Mito inayotoka Lukuga
Kimo cha uwiano wa maji juu ya UB 782 m
Miji mikubwa ufukoni Bujumbura, Kalemie, Kigoma
Ziwa Tanganyika pamoja na miji muhimu kando lake

Ziwa la Tanganyika ni kati ya maziwa makubwa ya Afrika ya kati ikiwa eneo lake ni la pili tu baada ya Viktoria Nyanza katika Afrika na ujazo wa maji yake ya pili duniani baada ya Ziwa Baikal.

Jina lake tangu 1919 limekuwa pia jina la koloni la Kiingereza la Tanganyika.

Ziwa lina ujazo wake mkubwa umetokana na vilindi vyake vinaelekea chini hadi mita 1470. Urefu wa ziwa ni 673 km na upana wake takriban 50 km. Maji ya Ziwa Tanganyika yanajaza ufa kubwa kwenye ganda la dunia ambalo ni sehemu ya bonde la ufa la Afrika ya Mashariki. Eneo la maji ni 32,900 km².

Ziwa la Tanganyika limepakana na nchi zifuatazo: Kongo, Tanzania, Burundi na Zambia. Kongo na Tanzania zinatawala sehemu kubwa ya ziwa.

Beseni ya ziwa ni 231,000 km². Mito miwili mikubwa ya Ruzizi na Malagarasi inapeleka maji yao ziwani. Maji yanatoka kwa njia ya mto Lukuga kwenda mto Kongo.

Miji mikubwa ziwani ni mabandari ya Kigoma kwa upande wa Tanzania na Kalemie kwa upande wa Kongo. Kila bandari ni pamoja na mwanzo wa njia ya reli. Mji mkubwa kabisa ni Bujumbura mji mkuu wa Burundi.

Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tanganyika (ziwa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.