Kalemie

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Sokoni ya Maendeleo

Kalemie ni mji wa J.K. Kongo uliopo kando la ziwa Tanganyika upande wa magharibi kwa kimo cha mita 785 juu ya UB pale ambako mto Lukuga unapotoka ziwani. Mwaka 2005 Kalemie ilikuwa na wakazi 147,000. Kuna bandari muhimu yenye mawasiliano kwa meli na Kigoma (Tanzania) na Bujumbura (Burundi).

Kalemie iliundwa kama kituo cha kijeshi tar. 30 Desemba 1891 upande wa kusini ya chanzo cha mto Lukuga ziwani na kapteni Mbelgiji Jaques de Dixmude kwa jina la Albertville kwa heshima ya mfalme mtarajiwa Albert wa Ubelgiji. Mji ulikiua baada ya kufika kwa reli ya Kongo.

Kalemie ni mwisho wa reli; mipango ya kale ya ukoloni ni ya kwamba njia ya reli kutoka Atlantiki ingeishia hapa itakayoounganishwa kwa feri na bandari ya Kigoma penye chanzo cha reli ya Tanganyika kwenda Daressalaam. Kutokana na miaka mingi ya fujo reli ya Kongo haikukamilishwa kamwe haifiki hadi Atlantiki lakini kuna njia ya reli kuanzia Kalemie hadi jimbo la Katanga.

Kuna viwanda vya nguo na saruji.

Mwaka 2005 mji uliathiriwa na tetemeko la ardhi lililosababisha uharibifu.

Flag-map of the Democratic Republic of the Congo.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kalemie kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.