Nenda kwa yaliyomo

PH

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

pH (ing. potential of hydrogen, pH value) ni kipimo cha kutaja kiwango cha asidi. Kuna skeli kuanzia 0 hadi 14. 0 ni asidi kali kabisa, 14 ni kinyume magadi matupu.

Asidi kali zaidi huwa na pH ndogo, myeyusho alikali zaidi huwa na pH ndogo. Dutu au mimumunyo zisizo kiasidi wala kialkali (ing. neutral solution) huwa na pH ya 7.

Asidi zina pH chini ya 7. Alikali au besi huwa na pH juu ya 7.

Kikemia pH ni kipimo cha uwingi wa protoni za (H+) katika mmumumnyo. Jina limetokana na Kilatini cha kitaalamu kwa "potentia hydrogeni" yaani nguvu (potentia) ya hidrojeni (H) au makini zaidi ioni za hidrojeni (H+).

Fomula kwa kukadiria pH ni:

[H+] inaonyesha kiwango cha ioni za H+ kwa kipimo cha moli kwa lita (ing. molarity).

Dutu ziliyo huwa na kipimo cha pH kati ya 0 na 14, lakini kuna pia dutu asidi au alikali sana zenye pH < 0 au pH > 14.

Dutu kialikali zina ioni nyingi za hidroksidi (OH-) badala ya ioni za hidrojeni.

Indiketa za pH

Indiketa ya pH ni kampaundi ya kikemia inayotiwa kwa kiasi kidogo kwenye mmumunyo na kubadilisha rangi yake. Ni njia ya kutambua na kuonyesha ioni za hidroni (H3O+) au ioni za hidrojeni (H+).Indiketa hizi hubadilisha rangi kulingna na kiwango fulaniu kwenye skeli ya pH.

Mbinu mwingine ni matumizi ya karatasi ya litmus inayobadilisha rangi kama kemikali ni zaidi kiasidi au zaidi kialikali lakini bila kuonyesha kiwango kikamilifu.

Mifano ya vipimo vya pH vya dutu mbalimbali

vipimo vya pH vya dutu mbalimbali
pH
Asidi ya beteri ya motokaa 1.0
Asidi ya tumboni 2.0
Maji ya limau 2.4
Cola 2.5
siki 3.0
Maji ya chungwa 3.5
Bia 4.5
Kahawa 5.0
Maziwa 6.6
Maji safi 7.0
Damu 7.35 - 7.45
Sabuni ya nywele (shampoo) 8.0
Maji ya bahari 8.0
Sabuni ya kawaida 9.0 - 10.0
Rangi ya kutia kwenye nywele 9.5 - 10.5
Ammonia ya kusafishia vyombo nyumbani 11.5
Dawa ya klorini 12.3
Maji magadi 13.5


Tazama pia

Marejeo

Viungo vya Nje