Kongo (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mto wa Kongo
Beseni ya mto Kongo
Chanzo Katika milima ya Mitumba takr. 100 km magharibi ya Lumbumbashi (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo)
Mdomo Atlantiki
Nchi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo
Urefu 4,700 km
Kimo cha chanzo 1,400 m
Tawimito Lufira, Kasai, Ubangi
Mkondo 42,000 m³/s
Eneo la beseni 3,730,000 km²
Idadi ya watu wanaokalia beseni milioni 56
Miji mikubwa kando lake Kisangani, Mbandaka, Kinshasa, Brazzaville, Matadi


Mto wa Kongo (kati ya 1971 and 1997 uliitwa Zaire) ni mto mkubwa wa Afrika ya kati. Ni mto mrefu wa pili katika Afrika baada ya Nile.

Beseni ya Kongo pamoja na tawimito yake ni eneo kubwa la pili duniani la msitu wa mvua. Pia kiasi cha maji pamoja na ukubwa wa beseni yake zina nafasiy a pili duniani baada ya Amazonas huku Amerika ya Kusini.

Jina la mto limepatikana kutokana na Ufalme wa Kongo uliokuwa dola kubwa katika Angola ya Kaskazini na Kongo ya Magharibi wakati wa karne 14-17 BK. Jamhuri zote mbili za Kongo zimepata majina yao kutoka kwa mto.

Mto wa Kongo ni njia muhimu ya mawasiliano na biashara kwa meli zinazoweza kusafiri mle kwa kushirikiana na njia za reli penye maporomoko mahali patatu.

Chanzo cha mto kipo karibu na mji wa Lumbumbashi katika jimbo la Katanga. Kwenye kilomita 1,800 za kwanza mto unaitwa Lualaba. Jina la Kongo latumiwa kuanzia mji wa Kisangani ambako mto umepita maporomoko ya Bayoma. Kuanzia Kisangani hadi Kinshasa mto ni njia ya maji inayopitiwa na meli za mtoni. Upande wa Lualaba kuna sehemu kadhaa zinazofaa kwa meli lakini njia ya maji inakatwa mara kadhaa na maporomoko.

Tawimito[hariri | hariri chanzo]

Tawimito inaorodheshwa kuanzia mdomo kulekea chanzo

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kongo (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.