Brazzaville

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Jiji la Brazzaville
Nchi Jamhuri ya Kongo
Kinshasa, Brazzaville na mto Niger

Brazzaville ni mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo. Ina wakazi 1,115,773 (mwaka 2005). Iko kando la mto Kongo ikitazama mji wa Kinshasa ng'ambo ya mto.

Jina la Brazzaville limetokana na Mfaransa Pierre Savorgnan de Brazza alinunua hapa ardhi kutoka kwa chifu Makoko na kujenga kituo kilichokua kuwa mji baadaye.

Tangu mwaka 1898 Brazzaville ilikuwa mji mkuu wa Kongo ya Kifaransa ikawa na na wakazi 5,000 mnamo 1900 walioongezeka kuwa lakhi moja mwaka 1950.

Mwaka 1940 Brazzaville ilikuwa kwa muda mfupi mji mkuu wa Ufaransa Huru yaani Ufaransa usio chini ya Ujerumani hadi kuhamia kwa serikali kwenda Algier.

Brazzaville ina bandari ya mtoni wa Kongo na mwanzo wa reli kuelekea pwani.

Vitabu[hariri | hariri chanzo]