Lomami (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Lomami ni tawimto mkubwa wa mto Kongo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwenye mwendo wa takriban 1500 km. Chanzo chake kiko katika kusini ya nchi kwenye jimbo la Katanga karibu na mji wa Kamina.

Lomami inajiunga na mto Kongo karibu na Isengi, takriban 150 km baada ya mji wa Kisangani kuelekea mdomo wa Kongo. Sehemu ya mwisho kabla ya mdomo wa Lomami inapitika kwa meli.