Ağrı

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wilaya ya Ağrı katika Uturuki.

Ağrı, zamani uliitwa Karaköse au Karakilise (kwa Kiarmenia: Արարատի; kwa Kikurdi: Agirî), ni mji mkuu wa Mkoa wa Ağrı uliopo mwishoni mwa mashariki ya nchi ya Uturuki, karibu kidogo na mpaka wa nchi ya Iran.

Uchumi na miundombinu[hariri | hariri chanzo]

Huu ni mkoa maskini wenye baridi kali mno, wengi wanaishi kwa kulisha mifugo yao katika maeneo ya milima. Kuna wanafunzi wachache sana wanaonweza kufika Chuo Kikuu, watu wanaolewa wakiwa bado wadogo, kuwa na familia ya watoto kumi au zaidi ni jambo la kawaida.

Mbunge wa huko Fatma Salman Kotan ameandika mahitaji yanayohitajika ili kuweza kuwasaidia wananchi wa mji huo.[1]

Wanajeshi wameweka kambi zao katika mhi huo na kuleta baadhi ya biashara kama migahawa ya chai na vyakula, pia inasemekana kuwa kunakuwa na kawaida ya uingizaji wa mali za magendo kwa kupitia mpaka huwa wa Iran.

Mji unaruhusu mahitaji ya msingi tu kama vile maduka ya dawa na mashule; kuna hitaji moja tu mbalo ndilo limeonekana la maana, ni mgahawa ambao watu wote hujumuika hapo kwa kunywa chai na kuvuta sigara.

Huko hakuna vilabu vya pombe, mabaa, wala majumba ya sinema. Kuna onyesho moja tu la sinema ambalo huonyeshwa katika moja kati ya mshule yaliyopo huko.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ağrı kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.