Nenda kwa yaliyomo

Bayburt

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha mji wa Bayburt

Bayburt (Kiarmenia: Բաբերդ, Baberd) ni mji mkuu wa Mkoa wa Bayburt katika nchi ya Uturuki.

Bayburt ulikuwa mji muhimu kabisa wakati wa zama za Barabara ya Hariri na pia mji ulipatwa kutembelewa na mpelelezi Marco Polo na msafiri wa Kituruki Evliya Celebi. Huko pia kuna mabaki ya ngome za Ufalme wa Byzantini.

Kuna misikiti kibao ya kuvutia, kuna mamawe kadhaa ya kituruki ikiwa sambamba kabisa na Miji ya Chini ya Catalcesme na pamoja na Maporomoko ya maji ya Sirakayalar.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Tarehe kamili ya kuanzishwa kwa mji huu wa Bayburt haijulikani. Ingawa, inakisiwa kwamba umeanzishwa kunako mwaka 100 KK. Mji wa Bayburt unafahamika zaidi kwa kuwa ulishawahi kumilikiwa na Dola la Roma na baada ya mgawiwo wa miji ukaja kuwa moja kati ya miji ya Roma ya Mashariki.

Wakati wa zama za Byzantini, Bayburt ulikuwa moja kati ya majimbo ya kujitawa ya Byzantine na uliitwa Heldia ukiwa kama wa 4 katika migawiwo yao ya miji saba iliyotengwa.

Mji pia unajulikana kwa ngome iliyorekebishwa na mfalme wa Byzantine maarufu kama Mfalme Justinia I, lakini baadaye mji ulipolwa na Waarabu. Waturuki walishikiria madaraka ya mji huo kwa mara ya kwanza mnamo 1054, na baada ya miaka 200 baadaye mji ukawa unashikiriwa na madola tofautitofauti.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]

Lua error in package.lua at line 80: module 'Module:Navbar/configuration' not found.