Nenda kwa yaliyomo

Eskişehir

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mji wa Eskişehir

Eskişehir (eskē'shehēr, Kituruki: Eskişehir, "Mji wa Kale"; Kilatini Dorylaeum; Kigiriki: Δορύλαιον, Dorylaeum) ni jiji lililopo kaskazini-magharibi mwa ya Uturuki na ndiyo mji mkuu wa Jimbo la Eskişehir.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2008, idadi ya watu wanaoishi katika mji imekadiriwa kufikia kiasi cha 614,247 ambao 599,796 wanaishi katikati ya jiji la Eskişehir.[1] Jiji lipo katika ukingo wa Mto Porsuk, takriban mita 792 kutoka juu ya usawa wa bahari, ambamo inatizama mapolomoko ya Phrygia.

Katika vilima vya karibu kuna visima vya maji ya moto. Takriban km 250 kutoka jiji hapa kuelekea mjini magharibi mwa Ankara, na km 350 kusini-mashariki ya jiji la Istanbul pia km 90 kutoka jiji hapa na kuelekea kaskazini-mashariki mwa mji wa Kütahya. Mji huu una eneo la kilomita za mraba zipatazo 2,678.[2]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Jina la mji la Eskişehir linamaa ya Mji wa Kale kwa lugha ya Kituruki, ingawa neno la kwanza la şehir linatokana na Kiajemi yaani neno shahr (Kiajemi: شهر), ina maana ya "mji". Mji hasa ulianzishwa na Waphrygia mnamo mwaka wa 1000 KK. Vinyago na masananmu mengi ya Waphrygia bado yanapatikana katika Majumba ya Sanaa ya Mambo ya Kale.

Pia kuna majumba ya maonyesho ya mawe ya meerschaum, ambazo shuhuli zake bado zinatamba hadi leo, ambavyo leo hii vinatumika kutengenezea kiko za kuvutia tumbaku zenye ubora hali ya juu. Mnamo karne ya nne AD, karibuni km 10 zilisogea kaskazini-mashariki mwa Karadja Hissar hadi Shehir Euyuk.

Muda wowote mji ukiwa unatajwa na wanajigrafia wa kale, basi walikuwa wakiuelezea kama moja kati ya miji mizuri ya Anatolia.

Kama jinsi ilivyo miji mingi ya Anatolia, Ukristo ulifikia baada ya Konstantine Mkuu aliyefanya kama dini rasmi ya Dola la Rom. Kuanzia karne ya nne, rekodi zilizopo zinaonyesha kwamba maaskofu wameanza kumiliki maofisi yao mjini Eski؛ehir. Hapo zamani mji ulikuwa ukijulikana kama Dorylaeum. Miongoni mwa maaskofu hawa, alikuwepo Eusebius, alikuwa akihusika sana na kuendeleza siri na itikadi ya kanisa.

ESTRAM (Eski؛ehir's tram service)

Utamaduni

[hariri | hariri chanzo]

Hali ya hewa

[hariri | hariri chanzo]

Eski؛ehir ni mji mkavu na wenye baridi, theuluji na joto, kiangazi. Mvua mara nyingi hutokea wakati bubujiko na kipupwe.

Months Jan Feb Mar Apr Mei Jun Jul Ago Sep Oct Nov Dec
Avr.Max. °C 3.9 6.2 11.2 16.4 21.8 25.9 29.2 28.9 25 19.8 12.4 5.5
Avr.Min °C -4.1 -3.9 -1.5 2.8 6.9 10.4 13.1 13 8.4 4.4 0.3 -2
Klabu Michezo Imeazishwa Ligi Uwanja
Eski؛ehirspor Mpira wa Miguu 1965 Turkcell Super League (Turkish Premier Division) Eski؛ehir Atatürk Stadium
Anadolu University Mpira wa Kikapu ? Turkish Basketball League 2 Anadolu University Sports Hall

Watu mashuhuri

[hariri | hariri chanzo]

Picha za mji huu

[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. TC Eskişehir Valiliği – Nüfus Durumu Ilihifadhiwa 28 Februari 2009 kwenye Wayback Machine. (Kituruki)
  2. Statoids. "Statistical information on districts of Turkey" (kwa English). Iliwekwa mnamo 2008-04-12.{{cite web}}: CS1 maint: unrecognized language (link)

Maelezo zaidi

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: