Bede Mheshimiwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Beda Mheshimiwa alivyochorwa katika Kumbukumbu za Nuremberg.
Kaburi la Beda katika kanisa kuu la Durham.

Beda Mheshimiwa (Wearmouth-Jarrow, leo nchini Uingereza, 672 au 67325 Mei - Wearmouth-Jarrow, 735) alikuwa mmonaki, padri, mwanateolojia na mwanahistoria nchini Uingereza.

Hasa anafahamika kwa kitabu chake “Historia ya kikanisa ya taifa la Waingereza” (kwa Kilatini: Historia ecclesiastica gentis Anglorum).

Mwaka 1899 alitangazwa na Papa Leo XIII kuwa mtakatifu na mwalimu wa Kanisa.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 25 Mei.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Karibu yale yote tunayoyajua kuhusu maisha ya Beda yamo katika sura ya mwisho ya Historia Ecclesiastica, aliyoimaliza mwaka 731 hivi, ambapo anadokeza kuwa yuko katika mwaka wa 59 wa maisha yake, hivyo alizaliwa 672–673.

Habari nyingine tunazipata katika barua ya mwanafunzi wake Cuthbert kuhusu kifo chake.

Beda hasemi kitu kuhusu asili yake, lakini kuna dalili kuwa familia yake ilikuwa na hali nzuri katika jamii.

Kumbe anataja mahali alipozaliwa kama "maeneo ya monasteri hii", yaani monasteri pacha ya Wearmouth na Jarrow.

Abati wake wa kwanza alikuwa Benedikto Biscop.

Alipofikia umri wa miaka 7, alitumwa monasterini ili apate malezi kutoka kwa abati huyo, halafu kwa Ceolfrith. Beda haelezi kama lengo la awali lilikuwa awe mmonaki baadaye. Lakini ndivyo ilivyotokea, akatumia maisha yake yote “kuimbia sifa za Mungu, kusoma, kufundisha na kuandika”, alivyosema mwenyewe.

Alipofikia miaka 19 tu, (692 hivi), alipewa daraja takatifu ya ushemasi, na alipofikia miaka 30 (702 hivi) alipata upadrisho.

Mtaalamu wa biolojia na historia, lakini hasa teoloja, alifaulu kufanya Biblia ieleweke kwa urahisi kupitia mahubiri yake sahili iliyofuata mfano wa mababu wa Kanisa.

Mwaka 701 hivi aliandika vitabu vyake vya kwanza, De Arte Metrica na De Schematibus et Tropis; vyote viwili kwa ajili ya madarasa.

Aliendelea kuandika maisha yake yote, akimaliza vitabu zaidi ya 60, vingi vikiwepo hadi leo.

Mwanashairi, aliandika tenzi kwa Bikira Maria ambazo ni kati ya zile bora zaidi zilizowahi kuandikwa.

Mwaka 708 baadhi ya wamonaki wa Abasia ya Hexham walimshtaki kuwa mzushi, lakini alifaulu kujitetea.

Mwaka 733 alisafiri hadi York, Lindisfarne na sehemu nyingine.

Alifariki tarehe 26 Mei 735 akazikwa Jarrow lakini masalia yake yakahamishiwa kwenye kanisa kuu la Durham katika karne ya 11.

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

 • Bede (1943). in Jones, C. W.: Bedae Opera de Temporibus. Cambridge, MA: Mediaeval Academy of America. 
 • Bede (2004). in Wallis, Faith (trans.): Bede: The Reckoning of Time. Liverpool: Liverpool University Press. ISBN 0-85323-693-3. 
 • Swanton, Michael James (trans.) (1998). The Anglo-Saxon Chronicle. New York: Routledge. ISBN 0-415-92129-5. 
 • Behr, Charlotte (2000). "The Origins of Kingship in Early Medieval Kent". Early Medieval Europe 9 (1): 25–52. doi:10.1111/1468-0254.00058. 
 • Brown, George Hardin (1999). "Royal and Ecclesiastical rivalries in Bede's History". Renascence 51 (1): 19–33. 
 • Cannon, John; Ralph Griffiths (1997). The Oxford Illustrated History of the British Monarchy. Oxford University Press. ISBN 0-19-822786-8. 
 • Farmer, David Hugh (1978). The Oxford Dictionary of Saints. Oxford, UK: Oxford University Press. ISBN 0-19282-038-9. 
 • Goffart, Walter A. (1988). The Narrators of Barbarian History (A. D. 550-800): Jordanes, Gregory of Tours, Bede, and Paul the Deacon. Princeton, N.J.: Princeton University Press. ISBN 0-691-05514-9. 
 • Higham, N. J (2006). (Re-)Reading Bede: The Historia Ecclesiastica in Context. Routledge. ISBN 978-0415353687. 
 • Opland, Jeff (1980). Anglo-Saxon Oral Poetry: A Study of the Traditions. New Haven and London: Yale U.P.. ISBN 0-300-02426-6. 
 • Thacker, Alan (1998). "Memorializing Gregory the Great: The Origin and Transmission of a Papal Cult in the 7th and early 8th centuries". Early Medieval Europe 7 (1): 59–84. doi:10.1111/1468-0254.00018. 
 • Ward, Benedicta (1990). The Venerable Bede. Harrisburg, PA: Morehouse Publishing. ISBN 0-8192-1494-9. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bede Mheshimiwa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.